Bariadi,
Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Mohamed Mchengerwa leo Disemba 18, 2023 amekabidhi magari 06 aina ya Land cruiser Hardtop kwaajili ya ufatiliaji wa shughuli mbalimbali za Afya Mkoa wa Simiyu.
Waziri Mchengerwa amekabidhi magari hayo wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu kwa ajili ya ukaguzi wa shughuli mbalimbali za maendeleo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi magari hayo Mhe.Mchengerwa amesema kwa sasa hategemei Waganga Wakuu waliopata magari hayo kukaa Ofisini badala yake wanapaswa wayatumie magari hayo kufanya ufatiliaji na kutatua kero mbalimbali zilizopo ngazi ya kata na vijiji ili sekta hiyo iweze kutoa huduma nzuri kwa wananchi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Dkt.Yahaya Nawanda ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha huduma za Afya Mkoani Simiyu ambapo amesema magari hayo yataongeza tija katika utoaji wa huduma za afya mkoa wa Simiyu
Halmashauri zilizopata magari hayo ni pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, na Halmashauri ya Wilaya ya Maswa.
GCO,
Simiyu RS
18 Disemba 2023.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa