Maswa,
Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISETA yamezinduliwa kimkoa leo 29 Mei, 2025 katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu Mhe.Faudhia Ngatumbura amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu katika uzinduzi wa mashindano hayo.
Akizungumza na washiriki wa mashindano hayo Mhe.Ngatumbura amesisitiza nidhamu katika kipindi cha makambi ya michezo hiyo pamoja na bidii ya mazoezi ili waweze kuleta ushindi katika ngazi ya Taifa jambo litakaloleta heshima kwa Mkoa.
Mwakilishi wa katibu Tawala Mkoa wa Simiyu katika uzinduzi huo ambaye ni Afisa Vijana Bi.Zena Mchujuko amesema vijana 120 watachaguliwa kuuwakilisha Mkoa katika ngazi ya Taifa kwa UMITASHUMTA pamoja na UMISETA.
GCU,Simiyu-RS
29 Mei,2025.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa