LENGO
Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji ina lengo la kutoa uwezeshaji wa kitaalamu kuhusu sekta za uchumi na uzalishaji kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Mkoa. Seksheni hii inaongozwa na Katibu Tawala Msaidizi ambaye anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa
Majukumu ya Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji
•Kuratibu utekelezaji wa sera za Kilimo, Mifugo, Ushirika, Misitu, Uhifadhi, Uvuvi, Viwanda, Biashara na Masoko katika Mkoa
•Kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Mkoa katika kutoa huduma kwenye nyanja za Kilimo, Mifugo, Ushirika, Misitu, Uhifadhi, Uvuvi, Viwanda, Biashara na Masoko
•Kuzisaidia na kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa juu ya teknolojia zinazofaa na za gharama nafuu katika sekta za uchumi na uzalishaji
•Kusajili vyama/vikundi vya ushirika katika Mkoa
•Kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa katika juu ya uanzishaji/uimarishaji na ukaguzi wa vyama vya Ushirika na Akiba na Mikopo
•Kusaidia na kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa juu ya kuzisimamia kampuni ndogo na za kati
•Kuzisaidia na kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutambua maeneo nyeti ya uwekezaji
•Kuzisaidia na kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuendeleza na kukuza sekta ya uvuvi na kuzalisha kisasa
•Kusimamia, kuratibu na kuwezesha masuala yanayohusiana na misitu katika Mkoa
•Kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa katika usimamizi wa sheria za kulinda wanyamapori
•Kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuendeleza maeneo ya wanyamapori
•Kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kusimamia utalii, idadi ya wanyamapori na mienendo yao/safari zao
•Kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutekeleza sheria ya Mazingira No. 2 ya mwaka 2004
•Kutoa ujuzi wa kitaalamu kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenye masuala yanayohusiana na maeneo/miradi ya umwagiliaji
•Kuratibu utekelezaji wa uboreshaji wa taratibu za biashara katika Mkoa
Seksheni inaongozwa na Katibu Tawala Msaidizi
Jina: Dkt. Gamitwe H. Mahaza
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa