Busega,
Walimu wa Somo la Hisabati wa Shule za Msingi Wilayani Busega Mkoani Simiyu wamepatiwa mafunzo ya umahiri kuhusu uboreshaji wa ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Hisabati.
Mafunzo hayo yanayoendelea katika ukumbi wa Shule ya Msingi Lukungu katika Kata ya Lamadi Wilayani humo ni muendelezo wa Mafunzo ya yaliyofunguliwa Tarehe 4 Septemba 2023 na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bw.Majuto Njanga
Mafunzo hayo yanayofadhiliwa na Mradi wa Shule Bora yana lengo la kuwajengea uwezo wa umahiri katika kuandaa mbinu rafiki za kuwasilisha maarifa ya somo hilo kwa wanafunzi, hatua itakayosaidia wanafunzi kupenda kujifunza somo hilo.
Kwa upande wao walimu wa somo la Hisabati waliopatiwa mafunzo hayo wameishukuru Serikali pamoja na Mradi wa Shule Bora Mkoani Simiyu kwa kuwapa maarifa na mbinu ambazo ni rafiki katika uhamasishaji, ufundishaji na ujifunzaji wa somo la hisabati.
Mafunzo hayo ya uboreshaji wa ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Hisabati kwa. Shule za Msingi Wilayani Busega yatamalizika Tarehe 8 Septemba 2023
GCO,
Simiyu RS
05/09/2013
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa