Bariadi,
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Dkt. Yahaya Ismail Nawanda amesema Mkoa wa Simiyu umejipanga vyema kuhakikisha kuwa Wananchi hususani wasiokuwa na uwezo Mkoani humo wanafikiwa na huduma ya msaada wa kisheria.
Dkt.Nawanda ameyasema hayo 18 Septemba 2023 wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya utoaji huduma ya Msaada wa kisheria kwa Wananchi ijulikanayo kama Kampeni ya Mama Samia ya Msaada wa kisheria,uliofanyika katika eneo la Stendi ya Zamani ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Katika kuunga Mkono Kampeni hiyo ya Mama Samia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt Yahaya Nawanda amesema Mkoa utatoa chumba maalumu kwa ajili ya Wataalamu wa Sheria kuhudumia Wananchi katika kila Ofisi za Kata na Kila kijiji mara baada ya Kampeni ya Mama Samia lengo likiwa ni kuhakikisha Wananchi wapatao Milioni 2.5 Mkoani Simiyu wanafikiwa na huduma hiyo muhimu.
"Tutatoa vyumba hivi bure kabisa na naomba nikuthibitishie Mhe.Waziri kuwa kuwa tumejipanga vyema katika kuhakikisha kuwa malengo mahsusi ya Kampeni ya Mama Samia yanatekelezwa kikamilifu ,kwetu hii ni fursa na naomba nikuhakikishie kuwa tunaenda kuvunja rekodi kwa kuwa na watu wengi zaidi na Simiyu tunakwenda kuwa wa kwanza"Alisema Dkt Nawanda.
Aidha Mkuu wa Mkoa Dkt Nawanda amemhakikishia Waziri wa Sheria na Katiba kuwa kama Mkoa watatoa ushirikiano mkubwa kwa Maafisa wote watakaoshiriki katika kampeni hiyo muhimu ili kufikia lengo la kuwafikia watu wengi zaidi Vijijini.
Amesema kuwa Mhe Rais ametoa huduma hiyo bure hivyo Wananchi wote wenye changamoto za kisheria mirathi,kijinsia na migogoro ya ardhi pamoja na matatizo ya mikataba kutumia hiyo fursa kwenda kupata huduma bure"alisisitiza Mkuu wa Mkoa Dkt Nawanda.
GCO,
Simiyu RS
18 Septemba 2023.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa