Bariadi,
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Dkt Yahaya Nawanda kwa kushirikiana na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoani Simiyu ameandaa ligi itakayojulikana kama Simiyu Super Cup ili kuleta Hamasa ya Michezo Mkoani humo.
Amethibitisha hayo 15 Septemba 2023 wakati wa Fainali ya mchezo wa mpira wa miguu iliyozikutanisha timu za Ikindilo FC na Kilulu FC katika Bonanza la Michezo lililoandaliwa na kituo cha Redio cha Bariadi FM katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Dkt Nawanda amesema uzinduzi wa Simiyu Super Cup unaobebwa na kaulimbiu inayosema “Tumekiwasha,Tumekufikia twende pamoja na Mama Samia” utafanyika siku ya Tarehe 18 Septemba 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambapo pamoja na uzinduzi litafanyika pia zoezi la ugawaji wa Vifaa vya Michezo kwa timu zinazoshiriki Ligi hiyo.
Ameongeza kuwa lengo la kuanzisha Ligi hiyo ni kuleta Hamasa ya michezo pamoja na kuibua vipaji katika mchezo wa mpira wa Miguu Mkoani Simiyu ili Vijana waweze kutumia fursa ya mchezo wa mpira wa miguu kunufaika kiuchumi.
Aidha Dkt Nawanda ameongeza kuwa Fainali za Simiyu Super Cup zitakazofanyika Mwezi Septemba 2023 katika uwanja wa Hamashauri ya Mji wa Bariadi zitapambwa na Wasanii wakubwa mbalimbali Nchini akiwemo Jux,Dulla Makabila pamoja Marioo.
GCO,
RS -Simiyu
15 Agosti 2023.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa