Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Dkt.Yahaya Nawanda akizungumza wakati wa hafla ya kuwakabidhi walimu iliyofanyika katika kata ya Kabita Wilayani Busega.
Na:IO Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Dkt.Yahaya Nawanda amewaagiza Viongozi Wilayani Busega kuhakikisha Walimu wanalipwa madai yao mbalimbali wanayodai kwa wakati ili kuleta ari ya Walimu kufanya kazi zaidi ili kuinua ubora wa Elimu.
Dkt.Nawanda pia amewaagiza Viongozi hao kuhakikisha watoto wote walioacha shule kutokana na sababu mbalimbali wanarejeshwa shule ili kuondoa tatizo la mdondoko wa Wanafunzi Wilayani humo.
Mhe Dkt.Nawanda ametoa maagizo hayo katika hafla ya kuwapongeza Walimu iliyofanyika katika Kata ya Kabita iliyoandaliwa na Diwani wa Kata hiyo Mhe. Silas Sosola kwa lengo la kuwapongeza Walimu kwa kazi kubwa waliyofanya ya kuinua ufaulu katika Kata hiyo.
Mhe.Nawanda emeeleza kuwa endapo walimu watalipwa madai yao kwa wakati na kuboreshewa maslahi yo itasaidia kwa sehemu kubwa kuinua ubora wa Elimu na hivyo kuongeza kiwango cha ufaulu wa Wanafunzi.
Ameeleza kuwa Serikali inachukua hatua mbalimbali kuboresha maslahi ya Walimu pamoja na watumishi wengine ambapo amempongeza Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa hatua anazochukua katika kuboresha maslahi ya watumishi wa Umma Nchini.
Aidha amempongeza Diwani wa Kata ya Kabita kwa kuandaa hafla ya kuwapongeza Walimu ambapo ametoa wito kwa viongozi wengine kuiga mfano wa Diwani huyo kuwapa motisha walimu ili kuamsha ari ya utendaji kazi kwa Watumishi hao
Katika Hafla hiyo pia Dkt.Nawanda amekabidhi Walimu wakuu wa Shule za Sekondari zilizofanya vizuri zawadi ya Shilingi laki tano kila mmoja pamoja na vyeti ikiwa ni pongezi kutoka kwa Diwani wa Kata ya Kabita kwa kuthamini mchango wa Walimu hao katika kuinua ubora wa Elimu katika Kata hiyo.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa