Pichani:Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Dkt.Yahaya Nawanda akimkabidhi Mwanafunzi Misana Salu Salilu wa Kidato cha tatu Shule ya Sekondari Ntuzu Bariadi,Baiskeli kwa ajili ya kumrahishishia usafiri ili kufika Shule kwa wakati
Na::GCO-Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Dkt Yahaya Nawanda leo 13 Mei 2023 amemkabidhi Baiskeli aina ya Phonex pamoja na Fedha Taslimu Shilingi Elfu Themanini na Sita kwa ajili ya Mahitaji mbalimbali ya shule Mwanafunzi Misana Salu Salilu wa Kidato cha tatu kutoka Shule ya Sekondari Ntuzu katika Halmashauri ya Mji Bariadi.
Misana ambaye kwa sasa anaishi na Bibi yake ambae ni Mlemavu amekabidhiwa zawadi hiyo ya Basikeli ili kumrahisishia kufika shuleni kwa wakati kutokana na kuishi mbali na Shule.
Akikabidhi zawadi hiyo Ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt.Nawanda amemsisitiza Mwanafunzi Misana kusoma kwa bidii ambapo pia ametoa wito kwa Jamii kujitolea kuwasaidia Wanafunzi waishio katika mazingira magumu.
Kwa Upande wake Mwanafunzi Missana Salilu baada ya kupokea zawadi hiyo amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa zawadi ya Baiskeli na Fedha Taslimu ambapo ameeleza kufarijika kwa msaada huo.
Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Mji Bariadi Bi.Hellen Mselle amemshukuru mkuu wa Mkoa ambapo ameeleza kuwa Usafiri huo utamsaidia Msichana huyo kwa ajili ya Usafiri wa kuwahi shule pamoja na kumsaidia Bibi yake kwa ajili ya shughuli ndogondogi kama vile kuchota maji na kazi nyingine ndogondogo.
Naye Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu Bw.Majuto Njanga ametoa wito kwa Jamii kusaidia watoto wenye uhitaji kwa kuwa kutoa ni Moyo na Sio Utajiri.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa