ATOA ZAWADI MBALIMBALI KWA VITUO VIWILI VYA YATIMA KWA AJILI YA SIKUKUU YA MWAKA MPYA 2024.
RC SIMIYU AKABIDHI ZAWADI HIZO KWA NIABA YAKE.
Busega,
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mh.Dkt Yahaya E. Nawanda amekabidhi zawadi mbalimbali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan katika vituo viwili vya kuelelea watoto Yatima Wilayani Busega Mkoani humo.
Dkt.Nawanda amekabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Mhe.Rais Dkt Samia ikiwa ni dhamira njema ya Mhe.Rais kuungana na Yatima,wasiojiweza na waishio katika Mazingira magumu Mkoani Simiyu katika kusherehekea Mwaka mpya 2024.
Vituo vilivyonufaika na Zawadi mbalimbali kwa ajili ya mwaka mpya kutoka kwa Mhe.Rais Dkt.Samia Mkoani Simiyu ni pamoja na Kituo Cha kulelea watoto yatima cha Bethany pamoja na Kituo Cha ulelea watoto Yatima Cha Kalemera vyote vya Wilayani Busega.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo Mkuu wa Mkoa Dkt Nawanda amewaambia watoto hao kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan anawapenda na kwba anaungana nao katika kusherehekea sikukuu hizo.
"Tunamshkuru sana Mhe.Rais kwa kutuchagua Mkoa wetu wa Simiyu kuwa miongoni mwa wanufaika wa zawadi hizi za Mwaka mpya kwa ajili ya Yatima na waishio katika Mazingira magumu"Alisema Mkuu wa Mkoa Dkt Nawanda.
Kwa upande wao watoto pamoja na Viongozi wa Vituo hivyo vya kulelea watoto Yatima Wilayani Busega wamemshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuwajali Kwa zawadi hizo kipindi hiki Cha sikukuu.
Zawadi zilizokabidhiwa ni pamoja na Mbuzi kadhaa kwa ajili ya kitoweo,Mchele,Maharage,Sukari,Unga wa Sembe,Juisi,Maji,Sabuni pamoja na Viunfo vya Chakula.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa