Dodoma,
Maafisa Serikalini kutoka mikoa 26 ya Tanzania Bara miongoni mwao wakiwemo Maafisa kutoka Mkoani Simiyu wapo katika mafunzo ya siku 5 ya mfumo mpya wa ununuzi wa umma (NeST) yanayotolewa na Mamlaka ya udhibiti wa ununuzi wa umma PPRA katika ukumbi wa PSSSF mjini Dodoma.
Maafisa waliohudhuria mafunzo hayo kutoka Mkoa wa Simiyu ni pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Sheria,Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi,Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA,Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, pamoja na Katibu Tawala msaidizi Sehemu ya usimamizi wa Serikali za Mitaa.
Mtendaji mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa ununuzi wa Umma PPRA Nchini Bw.Eliakim Maswi amesema Mafunzo ya mfumo mpya wa ununuzi wa Umma NesT yanafanyika kufuatia Serikali kupitisha Sheria mpya ya kuanza kutumika kwa mfumo huo mpya tangu Julai Mosi 2023.
Awali Serikali ilikuwa ikitumia mfumo wa TANEPS katika ununuzi wa Umma ambao ulibainika kuwa na changamoto mbalimbali hatua iliyopelekea Serikali kuachana na mfumo wa zamani na kuja na Mfumo mpya wa NeST ili kurekebisha changamoto zilizojitokeza na kuboresha Mfumo mzima wa ununuzi wa Umma Nchini.GCO,Simiyu -RS 01 August 2023.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa