NI KWA UFADHILI WA MRADI WA SHULE BORA,
WENYEWE WAKIRI MAFUNZO HAYO KUWA MWAROBAINI KUONGEZA UFAULU WA HISABATI.
Busega,
Walimu Wakuu wa Shule za msingi Wilayani Busega Mkoani Simiyu wamepatiwa mafunzo kuhusu Uboreshaji ufundishaji na Ujifunzaji wa umahiri wenye changamoto katika somo la Hisabati.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bw.Majuto Njanga Kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa Bi Prisca Kayombo ameyafungua mafunzo hayo ya siku 4 yanayofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Msingi Lukungu katika Kata ya Lamadi Wilayani humo.
Akizingumza wakati wa ufunguzi huo Kaimu Katibu Tawala Njanga amewataka walimu kuwa mfano katika kupenda somo la Hisabati Ili kuwavutia Wanafunzi nao waweze kuwa na moyo wa kujifunza somo hilo.
Amebainisha kuwa iwapo walimu watatumia mbinu rafiki katika Uboreshaji ufundishaji na Ujifunzaji wa somo hilo itasaidia kuongeza kiwango cha ufaulu wa Wanafunzi.
Awali Mratibu Msaidizi wa Shule Bora kwa upande wa Miradi inayofanya kazi na Wizara ya Elimu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw.Moses Mkotya, amewataka maafisa Elimu na Wakuu wa Shule waliyoshiriki mafunzo hayo, kwenda kuyatumia kuongeza ufaulu wa hisabati katika shule zao, kwa kuwaelimisha walimu wa hisabati mbinu za ufundishaji na kufuatilia utekelezaji wake.
Kwa upande wao Maafisa Elimu Kata na Walimu Wakuu, wameshukuru Mradi wa Shule Bora, wakisema umewapa maarifa na mbinu ambazo ni rafiki katika uhamasishaji na ufundishaji wa somo la hisabati.
GCO,
Simiyu-RS
04/09/2023.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa