MAADHMISHO YA SIKU YA USAFI WA MAZINGIRA DUNIANI MKOANI SIMIYU,
❇️RC SIMIYU AWAONGOZA WANANCHI KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA,
❇️AWAAGIZA WAKUU WA WILAYA/WAKURUGENZI KUSIMAMIA UTEKELEZAJI USAFI WA MAZINGIRA KILA MWEZI.
Bariadi,
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Dkt Yahaya Ismail Nawanda amewaagiza Wakuu wa Wilaya Mkoani Simiyu kuendelea kusimamia utekelezaji wa Shughuli za Usafi wa Mazingira kila mwisho wa Mwezi ili kuimarisha Usafi wa Mazingira Mkoani humo.
Dkt.Nawanda amewaongoza Wananchi na Watumishi kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali Mkoani humo kufanya Usafi wa Mazingira katika eneo la Hospitali ya Wilaya iliyoko Somanda Halmashauri ya Mji Bariadi katika kuadhimisha siku ya Usafi wa Mazingira Duniani.
Akizungumza na Wananchi pamoja na Watumishi katika eneo la Stendi ya mabasi yaendayo Mikoani Somanda mara baada ya usafi wa Mazingira Dkt.Nawanda ametoa rai kwa Wananchi kuendeleza utamaduni wa kufanya Usafi wa Mazingira kila mwisho wa wiki ili kuweka Mji katika hali ya Usafi.
"Maeneo mengine wamefanikiwa kuweka miji yao katika Hali ya Usafi hivyo ni muhimu na sisi mkoa wa Simiyu kuiga mifano mizuri katika maeneo mengine kwa kuendeleza utamaduni wa kufanya usafi wa mazingira kila Jumamosi Ili kuweka Mkoa wetu katika hali ya Usafi"Alisema Mkuu wa Mkoa Dkt. Nawanda.
Aidha Dkt.Nawanda pia amemuagiza mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Bariadi kuhakikisha Usafi wa vyoo katika Stendi hiyo.
Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Usafi wa Mazingira yanaadhimishwa kwa kila Mkoa Nchini chini ya kaulimbiu ya maadhimisho inayosema “Tumia mifuko mbadala wa Plastiki; kwa ustawi wa Afya, Mazingira na Maendeleo ya Uchumi”.
Kaulimbiu hii ni mwitikio wa Taifa wa Tamko la Serikali la kukataza uzalishaji, uingizaji ndani ya nchi usambazaji na matumizi ya mifuko ya plastiki na kuhimiza wananchi kutumia mifuko mbadala. Tamko hili limetokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaotokana na utupaji ovyo wa mifuko ya plastiki ambayo imeleta madhara makubwa ya kimazingira, afya za viumbe hai, ikiwemo binadamu wanyama, pamoja na kuathiri uchumi wa nchi kwa ujumla
GCO,
Simiyu RS
16 Septemba 2023.
www.simiyu.go.tz
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa