Pichani:Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa.
HISTORIA FUPI
Wilaya ya Maswa ni kati ya Wilaya 5 zinazounda Mkoa mpya wa Simiyu. Wilaya nyingine zinazounda Mkoa wa Simiyu ni Bariadi, Busega, Meatu na Itilima. Kwa upande wa Mashariki inapakana na Wilaya ya Meatu, Upande wa Kaskazini hadi Kaskazini Magharibi inapakana na Wilaya ya Itilima,Kusini hadi Kusini Magharibi inapakana na Wilaya ya Kishapu (Mkoa wa Shinyanga) na Upande wa Magharibi inapakana na Kwimba (Mkoa wa Mwanza).
Eneo la Wilaya ni kilometa za mraba 3,398 kati ya hizi 2,475 zinafaa kwa shughuli za kilimo na ufugaji, wakati kilometa za mraba 77 ni hifadhi ya misitu na kilometa za mraba 846 ni miinuko ya mawe, vilima na vichaka.
Kiutawala, Wilaya ina tarafa 3, Kata 36 Mamlaka ya Mji 1 yenye vitongoji 40, pia kuna vijiji 120, na vitongoji 510.Halmashauri ina jumla ya Divisheni 9 na Vitengo 9.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa kwa sasa ni Mhe.Aswege Kaminyoge.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa