LENGO
Kusimamia na kutoa huduma kwenye halmashauri husika kuhusu maendeleo ya sekta ya maji
Majukumu ya Seksheni ya Huduma za Maji
•Kutathimini, kuratibu na kushauri juu ya utekelezaji wa sera za sekta ya maji katika Mkoa
•Kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenye sekta ya Maji
•Kuwasiliana au kuwa daraja kuunganisha baina ya Mamlaka zinazohusika kwenye Serikali Kuu na Mamlaka za Serikali za Mitaa juu ya masuala yanayohusu sekta ya Maji
•Kuendeleza na kuboresha hali ya huduma za maji na usafi wa mazingira katika Mkoa
•Kuwezesha, kuratibu, Kusimamia, na kuthibiti sekta binafsi zinazotoa huduma za Maji katika Mkoa.
•Kuwezesha na kuratibu timu ya huduma za Maji na Usafi wa Mazingira katika Mkoa
•Kuzisaidia na Kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa kutambua na kuimarisha vyombo huru vya watumiaji maji
•Kuzisaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuandaa Miongozo ya utekelezaji na ukarabati wa miradi ya Maji
Seksheni hii ilikuwa ikiongozwa na Katibu Tawala Msaidizi
N.B Seksheni hii kwa sasa haiko chini ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, baada ya kuundwa kwa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Simiyu ni Mhandisi. Mariam Majala
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa