• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
OFISI YA MKUU WA MKOA WA SIMIYU
OFISI YA MKUU WA MKOA WA SIMIYU

.JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA .OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA OFISI YA MKUU WA MKOA WA SIMIYU

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Media Centre
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

SHULE 8 ZA MSINGI ZAPATIWA VIFAA VYA TEHAMA SIMIYU.

Posted on: April 20th, 2024

Bariadi,

Jumla ya Shule 8 za Msingi Mkoani Simiyu zimenufaika na vifaa mbalimbali vya TEHAMA vilivyotolewa na Serikali kupitia Mradi wa kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji kwa shule za Awali na Msingi Tanzania Bara (BOOST).

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anna Joram Gidarya amekabidhi vifaa hivyo leo 19 Aprili 2024 kwa wakuu wa shule za Msingi 8 zilizopata mgao wa vifaa hivyo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.

“Rai yangu kwenu ninyi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Dkt.Yahaya Nawanda,nendeni mkafanye kazi.Hii inaaonyesha ni jinsi gani Mhe.Rais anawathamini ninyi walimu”.Alisema Mhe.Gidarya.

Awali akizugumza na Maafisa Elimu pamoja na wakuu wa shule waliofika kwa ajili ya kukabidhiwa vifaa hivyo Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi.Prisca Kayombo ametoa rai kwa  Walimu waliopokea vifaa hivyo  kuvitunza  pamoja na kuvitumia kwa  kwa malengo yaliyokusudiwa.

Akisoma taarifa ya mapokezi ya Vifaa hivyo kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu Bw.Erasmus Buretta amesema Mkoa wa Simiyu kwa awamu ya kwanza ulipokea jumla ya Kopyuta za mezani 40,Printa 8 na UPS 24 na kusambazwa katika vituo 8 ambapo kwa awamu ya pili Mkoa umepokea jumla ya Kompyuta mpakato 16,Mashine  za Photocopy 8,Projecta 16,Skrini na Stendi 16,Smart TV za Nchi 65,Microphone 8,Zoom Camera 8,Digital Camera 8, na Wireless router 8.

Ameeleza kuwa tayari Walimu 16 na Maafisa TEHAMA 6 wa Halmashauri za Mkoa wa Simiyu wamepatiwa mafunzo ya namna ya kutumia vifaa hivyo yaliyofanyika Jijini Mwanza katika Chuo cha Ualimu Butimba Mwezi Februari 2024.

Kwa upande wao walimu pamoja na Maafisa Elimu walionufaika na Vifaa hivyo,wameishukuru Serikali kwa uwezeshaji huo ambapo wameahidi kutumia vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa.

Shule zilizonufaika na vifaa hivyo ni pamoja na Shule ya Msingi Nyakabindi,Ngulyati,Nyashimo,Luguru,Binza,Malampaka,Mwanhuzi pamoja na Mwabuma.

 

GCO,

Simiyu RS

19 Aprili 2024.

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 01, 2025
  • Fungua

Habari Mpya

  • SIMIYU RS WAHAMIA JENGO JIPYA LA UTAWALA NYAUMATA

    June 03, 2024
  • RC NAWANDA ARIDHISHWA NA UJENZI MRADI WA MAJI MWABUMA/MWASHATA MEATU.

    May 30, 2024
  • RC SIMIYU ARIDHISHWA NA MAENDELEO UJENZI WA MRADI WA USAMBAZAJI MAJI WA VIJIJI VYA SUNZULA, MWAMNEMA NA NGESHA WILAYANI ITILIMA,

    May 29, 2024
  • SHULE 8 ZA MSINGI ZAPATIWA VIFAA VYA TEHAMA SIMIYU.

    April 20, 2024
  • Fungua

Video

MIAKA MINNE YA RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN MKOANI SIMIYU
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • TUME YA RAIS UKUSANYAJI MAONI MABORESHO YA KODI YATUA SIMIYU
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii
  • SIMIYU- RS TV

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani
    • Video

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa