Bariadi,
Wananchi katika Halmashauri ya Mji Bariadi wameendelea kumiminika katika eneo la Stendi ya zamani kwa ajili ya kupatiwa huduma ya msaada wa kisheria katika kampeni ya Mama Samia Legal Aid Campaign inayoendelea Mkoani Simiyu.
Katika Banda la Wizara ya Katiba na Sheria(Pichani) Wataalamu wa masuala ya Sheria wanatekeleza wajibu wao kikamilifu kuwahudumia Wananchi wenye changamoto mbalimbali za kisheria.
Kampeni ya Mama Samia Legal Aid Campaign ilizindinduliwa 18 Septemba ,2023 na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Pindi Chana ambapo itadumu kwa muda wa Siku 10 tangu kuzinduliwa katika Wilaya zote 5 za Mkoa wa Simiyu.
GCO,
Simiyu RS
20 Septemba,2023.
www.simiyu.go.tz
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa