Bariadi DC,
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt.Yajaya E.Nawanda ameongoza Viongozi na Watendaji wa Halmashauri pamoja na Wataalamu wa Afya wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi katika ukaguzi wa Usafi wa Mazingira.
Dkt.Nawanda ameongoza operesheni hiyo katika mitaa mbalimbali ya Kata ya Dutwa kwa lengo la kukagua namna ambavyo Wananchi wa Halmashauri hiyo wanachukua hatua za kuweka Mazingira katika hali ya Usafi Ili kukabiliana na mlipuko wa magonjwa ya kuhara ikiwemo kipindupindu.
Katika operesheni hiyo Dkt.Nawanda ameonyesha kutoridhishwa na namna ambavyo Watendaji wa Serikali katika Kata hiyo wameshindwa kuhamasisha Usafi wa Mazingira katika eneo hilo.
Kufuatia Hali hiyo Mkuu wa Mkoa Dkt Nawanda ametoa wiki moja kwa Afisa Afya wa Kata ya Dutwa kuhakikisha kuwa Kata hiyo inakua safi muda wote na kwamba endapo akishindwa hatua Kali zitachukuliwa dhidi yake.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa