Itilima,
Wilayani Itilima Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Faidha Salim amewaagiza Wataalamu wa Afya kuhakikisha Elimu ya kujikinga dhidi ya Magonjwa ya kuhara ikiwemo kipindupindu inatolewa ipasavyo katika maeneo yote Wilayani humo ili kuepuka kusambaa kwa magonjwa hayo.
Ametoa rai hiyo alipokutana na kuzungumza na Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata na Vijiji,Wakuu wa Shule pamoja na Wakuu wa Idara na vitengo katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima.
Mhe.Faidha amewaagiza Watendaji wa Kata kuhakikisha kuwa Wanasimamia kikamilifu Usafi wa mazingira pamoja na kutoa hamasa ya ujenzi wa vyoo Bora katika maeneo yao ili kuepuka magonjwa ya kuhara pamoja na kipindupindu.
"Hakuna sehemu safi magonjwa ya kuhara na kipindupindu yanaweza kuingia,Usafi wa Jumamosi Watendaji tuzingatie.Na sio tu wikiendi hata Siku za kawaida"Alisema Mhe.Faidha
Maagizo hayo yanatolewa na Mkuu wa Wilaya ya Itilima kufuatia kuwepo kwa tishio la Mlipuko wa magonjwa ya kuhara ikiwemo kipindupindu katika baadhi ya maeneo Wilayani humo.
GCO,
Simiyu RS,
02 Januari 2023.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa