Bariadi,
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Dkt. Yahya Nawanda amewataka wakurugenzi wote na Maafisa Utumishi katika Halmashauri zote za Mkoa huo, kuhakikisha wanawasimamia walimu ipasavyo ili wasijiingize katika mikopo umiza.
Dkt.Nawanda ametoa maagizo hayo leo, wakati akifungua warsha ya siku ya moja ya Siku ya Mwalimu Mkoani humo ijulikanayo kama Mwalimu Spesho ambayo iliandaliwa na Benki ya NMB.
Amesema walimu wengi wameendelea kuteseka na taasisi ambazo siyo rasmi zinazojihusisha na utoaji wa mikopo, huku baadhi yao wakiamua kuacha kazi kutoka kuzidiwa na madeni.
Mwalimu anakopa hadi asilimia 100 ya mshahara wake, alafu wewe Afisa Utumishi upo ofisini na unaona, tunajua baadhi yenu mnahusika, nichukue nafasi hii kuwaonya, ukibainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yako,” ameongeza Dkt. Nawanda.
Katika Hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewataka na walimu kubadilika na kwenda katika taasisi ambazo ni rasmi ikiwemo benki ya NMB kwa ajili ya kupata mikopo yenye riba nafuu.
“ Hata sisi walimu tubadilike sasa, tuache kwenda kwenye hiyo mikopo umiza, NMB leo wamekuja na mikopo yenye riba nafuu kupitia kifurushi cha Mwalimu Spesho, tukitumia njia hii tutafanya kazi kwa amani,” amesema Dkt. Nawanda.
Aidha Dkt.ameipongeza NMB kwa kuona umuhimu wa kukutana na walimu na kuwapa elimu ya ujasliamali pamoja na kuwanoyesha huduma mbalimbali za mikopo inayotolewa na benki hiyo kupitia mfumo wa Mwalimu Spesho.
Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio amesema kuwa kada ya ualimu bado imeendelea kukubwa na changamoto kubwa ya kwenda kukopa katika taasisi za kifedha ambazo siyo rasmi na baadaye kukubwa na msongo mkubwa wa mawazo kutokana na mikopo wanayopata kuwa na riba kubwa.
Amesema kuwa Benki ya NMB baada ya kuona changamoto hiyo, iliamua kuanzisha utaratibu wa kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa kada hiyo kupitia mfumo wa Mwalimu Spesho ambayo inamwezesha Mwalimu kuondokana na mikopo umiza.
GCO
Simiyu RS
20 Septemba 2023.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa