• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Zoezi la Upigaji Chapa Mifugo Laongezewa Muda wa Mwezi Mmoja

Posted on: December 31st, 2017

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina ameongeza muda wa mwezi mmoja kwa Halmashauri hapa nchini kukamilisha zoezi la upigaji chapa mifugo na kuwataka watendaji wote wa Serikali wanaohusika kuhakikisha mifugo yote inapigwa chapa.

Waziri Mpina ameyasema hayo leo wakati wa kuhitimisha zoezi la upigaji chapa Kitaifa katika Kijiji cha Migato wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, zoezi ambalo lilianza rasmi Kitaifa mwezi Desemba, 2016 na kupangwa kukamilika Desemba 31, 2017.

“Kwa kuwa hadi sasa zoezi hili limetekelezwa kwa asilimia 38.5 kutokana na sababu mbalimbali, Mimi Luhaga Mpina Waziri wa Mifugo na Uvuvi kwa Mamlaka niliyopewa chini ya sheria ya Utambuzi, Usajili na ufuatiliaji wa mifugo ya mwaka 2010 na kanuni yake, ninaongeza muda wa kupiga chapa mifugo kutoka tarehe 01/01/ 2018 hadi 31/01/2018”alisititiza.

Mpina amesema miongoni mwa changamoto zilizopelekea Halmashauri nyingi kushindwa kutekeleza zoezi hilo kwa asilimia 100 ni baadhi ya halmashauri kutokutenga fedha kwa ajili ya zoezi hilo, kubaini mifugo kutoka nje ya nchi, baadhi ya wafugaji kushindwa kutaja idadi halisi ya mifugo yao na baadhi ya Halmashauri kuwatoza wafugaji zaidi ya shilingi 500 ambayo ndiyo bei elekezi, ambapo ameagiza wafugaji hao waliotozwa zaidi ya shilingi 500 warejeshewe fedha zao.

Ameongeza kuwa hadi kufikia Desemba 31, 2017  Halmashauri 30 hapa nchini hazijapiga kabisa chapa mifugo, halmashauri 23 zimeendesha zoezi hilo chini ya asilimia 10 na akaongeza kuwa orodha ya majina ya viongozi wa wilaya hizo walioshindwa kutekeleza agizo hilo la Serikali ameyawasilisha kwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa.

“Halmashauri 30 ambazo hazijapiga chapa kabisa hata ng’ombe mmoja na zile 23 ambazo zimepiga chini ya asilimia 10 majina  ya viongozi wote na Halmashauri husika nimekabidhi orodha hiyo kwa Waziri Mkuu, hatuwezi kuendekeza ukaidi wa maagizo ya Viongozi Wakuu wa Nchi” alisema Mpina.

Akiwasilisha taarifa ya zoezi la Upigaji Chapa katika Mkoa wa Simiyu, Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa, Ndg.Elias Kasuka amesema zoezi hilo mkoani humo lilianza rasmi mwezi Aprili 2017 ambapo hadi sasa ng’ombe zaidi ya 764, 933 wameshapigwa chapa kati ya ng’ombe 1,500,000.

Akitoa maoni yake baada ya kuhitimisha zoezi la upigaji chapa mifugo, Paulo Mabula mfugaji kutoka Migato Itilima amesema wafugaji wamelipokea kwa furaha agizo la Waziri wa Mifugo na Uvuvi kuongeza siku za kwa ajili ya kupiga chapa kwani litawasaidia wafugaji ambao bado hawajakamilisha ili kuondokana na changamoto ya wizi wa mifugo.

Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Itilima, Mhe.Mahamoud Mabula amemuomba Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.Luhaga Mpina kuwasaidia wafugaji wa Wilaya hiyo na maeneo mengine ya Mkoa huo kufanya vikao vya ujirani mwema na wale wa mikoa jirani ili kujadiliana namna ya kuondoa changamoto ya wizi wa mifugo.

 Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe.Benson Kilangi amesema viongozi na wataalam wa wilaya hiyo wamekuwa wakiwahamasisha wafugaji kupanga matumizi bora ya ardhi ili waweze kutenga maeneo kwa ajili ya malisho na kuyawekea miundombinu muhimu kwa ajili ya mifugo ikiwemo maji, majosho pamoja malisho

Vijana wa Skauti wilaya ya Itilima wakimvisha skafu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina alipowasili wilayani humo kwa ajili ya kuhitimisha zoezi la upigaji chapa mifugo kitaifa, mkoani Simiyu.

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akisalimiana na Afisa Mifugo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Ndg.Ally Mzee mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa ajili ya kuhitimisha zoezi la upigaji chapa mifugo Kitaifa, lililofanyika katika kijiji cha Migato wilayani Itilima.


Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi (wa tatu kushoto) akipiga chapa ng’ombe katika hitimisho la zoezi la upigaji chapa mifugo Kitaifa katika Kijiji cha Migato, Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu ambalo limehitimishwa na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Mhe.Daudi Nyalamu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Migato na vijiji jirani  mara baada ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina kuhitimisha zoezi la upigaji chapa mifugo Kitaifa lililofanyika kijijini hapo leo.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.Luhaga Mpina akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Migato na vijiji jirani  mara baada ya kuhitimisha zoezi la upigaji chapa mifugo Kitaifa lililofanyika kijijini hapo leo.

Mbunge wa Jimbo la Itilima, Mhe.Njalu Silanga akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Migato na vijiji jirani  mara baada ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina kuhitimisha zoezi la upigaji chapa mifugo Kitaifa lililofanyika kijijini hapo leo.

Ndg.Paulo Mabula akitoa mchango wake mara baada ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina kuhitimisha zoezi la upigaji chapa Kitaifa katika Kijiji cha Migato wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu.

 Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akisalimiana na Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Elias Kasuka mara baada ya kuwasili Mkoani humo kwa ajili ya kuhitimisha zoezi la upigaji chapa mifugo Kitaifa, lililofanyika katika kijiji cha Migato wilayani Itilima.

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akipokelewa na Viongozi wa Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu mara baada ya kuwasili wilayani humo kwa ajili ya kuhitimisha zoezi la upigaji chapa mifugo Kitaifa, lililofanyika katika kijiji cha Migato wilayani Itilima.


Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa