Akikabidhi vitabu hivyo kwa Maafisa Elimu wa Halmashauri zote sita za Mkoa wa Simiyu, Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka amesema vitabu hivyo ni msaada mkubwa kwa Mkoa huo, vikitumiwa vizuri na walimu wenye nia ya kufanya mapinduzi ya elimu na kuwasaidia wanafunzi kujua maana halisi ya vitabu hivyo, vitasaidia Mkoa wa Simiyu kufikia malengo ya kiushindani katika Elimu.
Ameongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata vitabu pamoja na mahitaji mengine ikiwa ni pamoja na madawati, walimu, vyumba vya madarasa vinavyotolesheleza hivyo akasisitiza vitabu hivyo vikatumike kwa kusoma ili viwasaidie.
“Vitabu hivi mtakapogawiwa mkavitumie kwa ajili ya kusoma visiwe mapambo na kama mwanafunzi hujui uliza, jibidiishe kujua kitabu hicho kinahusu nini na kama hujaelewa muulize mwalimu ili kesho kwenye mtihani ufaulu kama wenzako wananvyofaulu” alisema Mtaka.
Aidha, Mtaka amewataka Maafisa Elimu mkoani humo kuzungumza na walimu kabla ya kugawa vitabu hivyo ili vitakapogawiwa katika shule vigawiwe katika utaratibu mzuri utakowawezesha walimu kuwasadia wanafunzi kuvitumia kwa manufaa.
Akitoa taarifa juu mapokezi ya vikao hivyo Katibu Tawala Mkoa amesema Mkoa huo umepokea jumla ya vitabu 16,000 kwa ajili ya wanafunzi na vitabu 985 kwa ajili walimu(kiongozi cha mwalimu).
Akizungumza kwa niaba ya Maafisa Elimu Sekondari mkoani humo, Afisa Elimu Sekondari wa Halmahauri ya Mji Bariadi Mwl. Esthom Makyara amesema vitabu hivyo ni msingi mzuri kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza na Maafisa Elimu hao wanapaswa kuwaelekezaWakuu wa shule kutofungia vitabu hivyo stoo badala yake wanafunzi wapewe ili wavisome.
Naye Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Ndg.Charles Maganga amesema Maafisa Elimu Sekondari wahakikishe vitabu hivyo vinagawiwa kwa wakuu wa shule kabla ya shule kufunguliwa Januari 08, 2018, ili wanafunzi wa kidato cha kwanza wanapoanza masomo wavikute shuleni.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Bariadi walioshuhudia zoezi la ugawaji wa vitabu hivyo kimkoa wamesema, vitabu hivyo vitawasaidia wenzao wa kidato cha kwanza kujenga msingi mzuri wa maarifa ya jumla na lugha ya Kiingereza.
Vitabu hivi vimetolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Msaada wa Watu wa Marekani(UKAID) kupitia Mpango wa Taifa wa Kuinua Ubora wa Elimu hapa nchini EQUIP-T.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa