Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.David Kafulila amemuelekeza Katibu Tawala Mkoa Simiyu Bi. Prisca Kayombo,kuwataka wakurugenzi wa Itilima na Maswa kujieleza kufuatia kuchelewa utekelezaji miradi ya ujenzi wa madarasa chini ya mpango wa UVIKO-19.
" Nawapongeza Halmashauri za Bariadi mjini na vijijini kwa kufikia asilimia 90% ya utekelezaji. Pia Nawapongeza Meatu kufikia asilimia 72% na ninawaweka kiporo Busega walio asilimia 36%. Lakini kwa Wakurugenzi wa Maswa na Itilima nataka maelezo ya maandishi kwanini, ujenzi katika maeneo yenu upo chini ya asilimia 10% mpaka sasa ni jambo lisiloingia akilini, naelekeza RAS uwandikie barua " Amesema Mhe.Kafulila.
Aidha ameelekeza wakurugenzi na wakuu wa wilaya husika kuhakikisha wanafunga taa na ujenzi kuendelea usiku na mchana ili kuhakikisha Disemba 15 madarasa yanakabidhiwa tayari kutumiwa na wanafunzi.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa