Mwakilishi wa Wheelchair Foundation ya nchini Marekani Charli Butterfield amekabidhi baiskeli 48 kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka kwa ajili ya watu wenye ulemavu mkoani hapa.
Awali akipokea baiskeli hizo Mtaka ameishukuru taasisi hiyo kwa msada huuo na kutambua mahitaji ya watu wenye ulemavu ambao wanakabiliwa changamoto ya vifaa saidizi, huku akibainisha kuwwa mkoa utaendeleza uhusiano na shirika hilo..
Kwa upande wake mwakilishi wa Taasisi ya Wheelchair Foundation Charli amesema utoaji wa vifaa saidizi vya walemavu ni endelevu na shirika hilo limetoa zaidi ya baiskeli 4000 katika nchi mbalimbali Barani Afrika.
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo ameshukuru shirika la Wheelchair Foundation kwa msaada wa baiskeli kwa watu wenye ulemavu na kubainisha kuwa jamii ya wana Simiyu itaendelea kuwakumbuka.
Mmoja wa watu wenye ulemavu aliyenufaika na baiskeli akishukuru kwa niaba ya wenzake amesema baiskeli hizo zitawasaidia sana kama kifaa saidizi kwao maana awali ilikuwa inawalazimu kujongea kutoka eneo moja kwenda eneo jingine kwa shida.
MWISHO
KUPATA HABARI KAMILI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/07/wheelchair-foundation-yakabidhi.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa