• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Waziri Tizeba: Waandaaji Nanenane Andaeni Maonesho Yatakayosaidia Wananchi Kuleta Tija Katika Uzalishaji

Posted on: August 3rd, 2018

Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba amewataka Waandaaji wa Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima Nanenane hapa nchini kuhakikisha kuwa kuanzia mwaka 2019 wanaandaa maonesho hayo katika sura mpya itakayoleta mabadiliko chanya kwa wakulima, wafugaji na wavuvi ili waweze kuzalisha kwa tija.

.

Waziri Tizeba ameyasema hayo Agosti 03, 2018 katika Uwanja wa Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki, uliopo Nyakabindi Bariadi, wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 yanayofanyika Mkoani Simiyu.

Amesema ni vema waandaaji hao wakatoka katika maonesho ya mazoea ya kuwaonesha wakulima na wadau  vipando mbalimbali pasipo kuwapa elimu ya namna yakufikia uzalishaji wanaouona katika maonesho, badala yake maonesho hayo yatumike kuwafundisha wananchi na kubadilishana uzoefu.

“Kuanzia nanenane ya mwaka huu na zinazofuata, wandaaji wazipe sura mpya hata tunapowaomba wadau mbalimbali kuchangia maandalizi wawe wananamini kuwa tutakachokifanya kitaleta  mabadiliko chanya kwa wakulima, wafugaji na wavuvi wa nchi hii”alisema Tizaba.

 

Aidha, Dkt. Tizeba amekubaliana na mpango wa viongozi wa Mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga kufanya maonesho kila baada ya miezi mitatu katika Uwanja wa Nyakabindi ili kuwapa fursa wananchi ya kuendelea kujifunza badala ya kusubiri kila wiki ya nanenane kila mwaka.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema dhamira ya Mkoa huo na kanda ya Ziwa ya Mashariki ni kuendelea kufanya maonesho Teknojia za Kilimo  Biashara katika Uwanja wa Nyakabindi jambo ambalo litawapunguzia Watanzania kwenda nje ya nchi kujifunza teknolojia hizo.

“Tutafanya maonesho hapa kila baada ya miezi mitatu, kupitia maonesho yatakayofanyika eneo hili, tutawapunguzia wananchi safari za kwenda nje ya nchi  kufuata teknolojia za kilimo Biashara” alisema Mtaka.

Katika hatua nyingine Mtaka amesema Waoneshaji waliopo Uwanja wa Nanenane Nyakabindi wameomba kuongezewa siku mpaka kufikia Agosti 11 badala ya Agosti 08 kama ilivyo kawaida, jambo ambalo lilikubaliwa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles Tizeba.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima amesema matarajio ya viongozi wa Kanda ya Ziwa Mashariki ni kuyafanya maonesho ya nanenane kanda hiyo kuwa mnara wa mafanikio katika sayansi na teknolojia na namna ambavyo kilimo kinachozingatia kanuni bora kinavyochangia mabadiliko chanya ya mfumo wa Watanzania waanotegemea kilimo.

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba ametoa wito kwa wananchi kufika Uwanja wa Maonesho ya Nanenane Nyakabindi ili kupata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali kwa kuwa kwa sasa waoneshaji wa teknolojia mbalimbali wapo uwanjani hapo.

  

Maadhimisho ya Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima Nanenane mwaka 2018 yanayofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu ni ya 25 kufanyika hapa nchini na Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba amesema maonesho hayo yatafanyika miaka mitatu mfululizo, mwaka 2018, mwaka 2019 na mwaka 2020.

MWISHO

KUPTA PICHA ZAIDI KUHUSU UFUNGUZI WA NANENANE KITAIFA MWAKA 2018 FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/08/waziri-tizeba-waandaaji-wa-nanenane.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa