Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amewataka wakulima kuchangamkia fursa ya kilimo cha mbogamboga ili waweze kujipatia kipato kupitia kilimo hicho cha bustani ambacho uandaaji wake wa mashamba ni wa nafuu lakini kimekuwa na faida kubwa.
Mhe. Waziri Mkuu ameyasema hayo Agosti 08, 2020 wakati akihitimisha Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 yaliyofanyika kanda ya ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
Aidha, Mhe. Waziri Mkuu amewahimiza wakulima kuchangamkia mikopo inayotolewa na taasisi za kifedha ili waweze kupata mitaji itakayowasaida kuendesha shughuli za kilimo ikiwemo kilimo cha bustani, ufugaji na uvuvi.
Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga amesema katika upande wa chanjo na uhimilishaji serikali imeweka bei elekezi ya uhimilishaji ambapo kwa sasa Ng’ombe mmoja atagharimu kiasi cha 10,000 badala ya sh.25,000 ambapo katika maonesho ya nane nane ambapo msimu huu Wizara hiyo imeweza kuhimilisha Ng’ombe zaidi ya 100 bure .
Naye Waziri wa Kilimo Japheti Hasunga amesema kwa sasa Wizara ya kilimo imejikita kuhamasisha wakulima kutoka katika kilimo cha kujikimu na kuhamia katika kilimo cha Biashara na tayari Wizara hiyo imeanzisha huduma za ugani ambazo zitatolewa huku Jengo la Wizara ya kilimo lililopo ndani ya Viwanja vya Nyakabindi likipangwa kutumika kutoa mafunzo mwaka mzima,ambapo amaewaomba viongozi wa Mikoa husika kuhakikisha wanaleta wakulima ili wapate mafunzo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mkoa wa Simiyu umekuwa ukifanya vizuri katika kilimo cha zao la pamba hivyo akaomba serikali kuona namna ya kusaidia katika uongezaji wa thamani wa zao hilo, ambapo amekizungumzia kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba kinachotakiwa kujengwa wilayani Bariadi.
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/08/waziri-mkuu-awataka-wakulima.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa