• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Waziri Mhagama Azitaka Halmashuri Kuhakiki Taasisi Ndogo za Fedha Kubaini Taasisi Zinazowaibia Wananchi

Posted on: October 20th, 2019

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu , Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Jenista Mhagama , ameziagiza halmashauri zote nchini kufanya uhikiki wa kina wa taasisi ndogo za kifedha zinazotoa mikopo kwa wananchi na vikundi, ili kuzibaini taasisi zinazowaibia Watanzania badala ya kuwanufaisha kiuchumi..

Waziri Mhagama ametoa agizo hilo, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, yaliyofanyika Kitaifa katika  Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Oktoba 20, 2019.

“Ninajua baadhi ya taasisi ndogo za fedha badala ya kuwasaidia  wanachama zimekuwa ziifanya kazi ya kuiba fedha za wanachama  na kuwafanya wanachama warudi nyuma badala kusonga mbele, agizo hili Baraza la Taifa la Uwezesheshaji wananchi Kiuchumi mlifuatilie kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI,” alisema Mhagama.

Katika hatua nyingine ameitaka mifuko/programu za uwezeshaji wanachi kiuchumi kutoa mikopo kwa riba nafuu tofauti na taasisi nyingine za kifedha, ambapo amebainisha kuwa takribani wajasiriamali 1,237,984 wamenufaika na mikopo ya mifuko hiyo na hadi kufikia Juni 2019 jumla shilingi bilioni 388.4 zimetolewa.

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga ametoa wito kwa Taasisi za kifedha kuhakikisha zinajibu changamoto za wananchi huku akiwataka wananchi (wajasiriamali) walioshiriki maonesho haya kutumia vema fursa walizoziona katika mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ili wakuze uchumi wao

Baadhi ya wanufaika wa mikopo wilaya ya Bariadi na Busega mkoani Simiyu na Chato Mkoani Geita wamezishukuru Taasisi za kifedha zilizowakopesha mitaji jambo ambalo limewasaidia kuimarsisha shughui zao za kiuchumi wanazofanya ikiwa ni pamoja na kilimo na ufugaji.

“Naishukuru Benki ya AZANIA na wadhamini wangu Taasisi ya PASS kwa kuniwezesha kupata mkopo wa shilingi milioni 20, kuanzia sasa nitalima kisasa na nitaenda kuongeza miundombinu ya maji kwenye shamba langu maana nilikuwa nalima ekari 10 kwa kumwagilia badala ya ekari 30 nilizo nazo,” alisema Elisha Malugu kutoka wilayani Busega.

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi(NEEC) Dkt. Festus Limbu amesema NEEC inaendelea kufuatilia agizo la Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa alilolitoa Juni 2019 la kila mkoa kuwa na kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi, lengo likiwa kuvifanya vituo hivyo kuwa kitovu cha uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Katibu Mtendaji wa NEEC, Bi. Beng’ Issa amesema Maonesho haya yameshirikisha Taasisi 45, wajasiriamali zaidi ya 200 kutoka mikoa ya Simiyu, Mbeya, Pwani, Mwanza, Tabora, Kagera , Mara, Singida na Dar es Salaam na kutoka nchi jirani za Burundi na Kenya.

Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii chini ya Kauli Mbiu, “Mitaji ni Chachu ya Kujenga Uchumi wa Viwanda” yametanguliwa na maonesho ya kwanza yaliyofanyika Mbeya mwaka 2017, ambapo ya pili yalifanyika mwaka 2018  jijini Dodoma.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/10/waziri-mhagama-azitaka-halmashuri.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa