• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Waziri wa Ujenzi Amtaka Mkandarasi wa Barabara ya Bariadi-Maswa kukamilisha Ujenzi Juni 2019

Posted on: February 17th, 2018

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa amemuagiza Mkandarasi wa Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Bariadi-Maswa yenye urefu wa Kilomita 49.7 kukamilisha mradi huo Juni 2019.

Waziri wa Mbarawa amesema hayo wakati alipotembelea Kambi ya Mkandarasi CHICCO anayetekeleza Mradi huo iliyopo kata ya Luguru wilayani  Itilima wakati wa Ziara yake Mkoani Simiyu .

Amesema barabara hiyo iliyopangwa kujengwa kwa miezi 24 kuanzia Mwezi Oktoba 2017,  itajengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 86.9 na tayari Serikali imeshamlipa Mkandarasi shilingi Bilioni 8.9.

Amemuelekeza Mkandarasi CHICCO kutekeleza ujenzi wa barabara hiyo na  kuahidi kuwa Serikali itamsimamia na kuhakikisha mradi huo unakamilika mwezi Juni 2019, jambo ambalo limekubaliwa na Mkandarasi huyo.

“Tutahakikisha tunamsimamia Mkandarasi  masaa yote usiku na mchana ili barabara hii imalizike kwa wakati na tutamlipa fedha kila anapoleta ‘certicate’ kazi hii isisimame tena, nawaagiza TANROADS na Mkandarasi Mshauri kusimamia barabara hii ili thamani ya fedha ionekane” alisema Mbarawa.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ameshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli kutekeleza ahadi aliyoitoa mwezi Januari 2017 katika ziara yake Mkoani humo, ambapo amebainisha kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kutaufungua Mkoa huo kibiashara.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo ameshukuru juhudi zinazofanywa na Serikali kwa mkoa huo kwa kuwa ulipoanzaishwa mwaka 2012 barabara zilikuwa zinapitika kwa shida,  lakini sasa wananchi wanatumia muda mfupi kwenda maeneo mbalimbali, hivyo amesema barabara hiyo itakapokamilika nayo itachangia kurahisisha usafirishaji.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wa Kijiji cha Banya wilayani Itilima mahali inapojengwa Kambi ya Mkandarasi CHICCO wamelalamikia suala la mkandarasi kuchukua vibarua wa kufanya kazi za mradi nje ya Mkoa pamoja na malipo yasiyoridhisha  kwa wale waliopata nafasi ya kufanya kazi katika mradi huo

“Mhe.  Waziri hivi ni  sahihi kweli barabara ijengwe hapa kwetu halafu vibarua watoke Mikoa mingine, mimi naona siyo sawa  tunaomba Serikali itusaidie na sisi wananchi wa hapa tupate kazi; pia hata hawa wanaofanya kazi hapa malipo ni kidogo elfu tano kwa siku haitoshi” alisema Samweli Jisena.

Waziri Mbarawa amemuagiza Meneja wa TANROADS Mkoa wa Simiyu, Mhandisi.Albert Kent kuhakikisha kuwa anasimamia suala la wananchi wa eneo la mradi kupewa kazi na mkandarasi na upande malipo amewataka wafanyakazi kukubaliana na mkandarasi juu ya malipo yao.

Ujenzi wa Barabara ya Bariadi-Maswa ni ahadi ya Rais wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa Januari 11, 2017 akiwa katika ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu mara baada ya kufungua barabara ya Lamadi-Bariadi yenye urefu wa Kilomita 71.8 mjini Bariadi.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII FUNGUA HAPA:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/02/waziri-mbarawa-amtaka-mkandarasi-wa.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa