• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Waziri Mahiga Avitaka Vyombo vya Utoaji Haki Kuamua Kesi kwa Wakati Kuepuka Msongamano wa Mahabusu Magerezani

Posted on: July 14th, 2019

Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Augustine Mahiga amevitaka vyombo vya utoaji haki hapa nchini ikiwemo jeshi la polisi na Mahakama kutochelewesha utoaji wa haki ili kuepuka msongamano wa mahabusu katika magereza  na badala yake vyombo hivyo vitende  haki na kwa wakati.

Waziri Mahiga ameyazungumza hayo leo Julai 14, 2019 wakati akizungumza na waandishi wa habari Mjini Bariadi mara baaada ya kuhitimisha ziara yake na Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka, Biswalo Mganga mkoani Simiyu ambayo ililenga kujionea mazingira ya utoaji haki na haki jinai katika mikoa ya Simiyu na Mara.

“Kuna ucheleweshaji wa kutoa haki kabla mahabusu hajapelewa mahakamani, unaweza kuwa miezi sita, mwaka mmoja na wengine hata miaka miwili bado wanasubiri kwenda mahakamani; hilo nalo linachangia si tu uchache na nafasi ndani ya gereza lakini pia utaratibu wa upelelezi unachelewa ili kukamilisha mashtaka,lakini pia kazi za mahakimu zinatakiwa ziende haraka ili kupunguza mrundikano wa kesi” alisema Waziri Mahiga.

Aidha, Dkt. Mahiga amesema katika ziara hiyo pia wamebaini kuwa katika mikoa ya Simiyu na Mara mahabusu wengi wanakabiliwa na kesi za kuingilia hifadhi ya Taifa ya Serengeti, wizi wa mifugo, ugomvi utokanao na wizi wa mifugo na matatizo yatokanayo na jamii.

Ameongeza kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga  kwa mamlaka aliyopewa na sheria ya kusamehe baadhi ya makosa kwa utaratbiu na vigezo Fulani, katika kila Gereza walilopita DPP aliweza kuwasamehe baadhi ya mahabusu kwa kuzingatia vigezo kadhaa ambavyo ni wazee waliozidi miaka 70, watoto chini ya miaka 18, watu wenye ulemavu na wale wenye makosa madogo kama wizi wa kuku na wamekaa mahabusu kwa muda mrefu.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka(DPP), Biswalo Mganga  amesema pamoja na vigezo vilivyotajwa na waziri Mahiga baadhi ya wahabusu walioachiwa ni wale waliopelekwa gerezani au mahakamani wakati hawakustahili ikiwa ni pamoja na wale  waliobambikiwa kesi.

“Kwa hapa Bariadi kuna kesi 46 ambazo zina watu wanaoweza kufika 100, Tarime nako ni watu wengi kidogo lakini idadi haitusaidia, itoshe kusema kuna watu walioachiwa baada ya kuangalia vigezo fulani; kuna watu wanapelekwa mahakamani ambao pengine hawakustahili, ni kwa sababu ya kubambikiwa kesi, mfano mtu amekopa fedha na baada ya kushindwa kulipa badala ya kupelekwa kwenye kesi ya madai, mdai anampeleka polisi kumshtaki kwa kujipatia fedha kwa udanganyifu” alisema DPP.

Kwa upande wake mmoja wa wananchi Mjini Bariadi, Hangi Sapoti amesema ili kuzuia msongamano katika magereza ameshauri mahakama na jeshi la polisi kujiridhisha kabla ya kuwapeleka mahabusu gerezani na ikiwa watuhumiwa wamefanya makosa yanayoruhusu kupewa dhamana wapewe ili wabaki wale tu ambao wamefanya makosa yasiyo na dhamana.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/07/waziri-mahiga-avitaka-vyombo-vya-utoaji.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa