Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR-TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo amewaagiza Wakuu wa Mikoa nchini kuweka mpango mkakati wa kuwahamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ulioboreshwa kama alivyofanya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka, ili kuwapunguzia gharama za matibabu.
Mhe. Jafo alitoa agizo hilo wilayani Busega mkoani Simiyu katika hafla ya kupokea Majengo ya wodi ya wazazi na chumba cha upasuaji katika Kituo cha Afya NASA, ikiwa ni moja ya vituo vya Afya 38 mkoani Simiyu, pamoja na magari tisa yakiwepo magari matatu ya kubebea wagonjwa (Ambulance) na magari Sita kwa ajili ya uratibu wa huduma za Afya yaliyopatikana chini ya ufadhili wa UNFPA/KOICA , msaada uliogharimu jumla ya shilingi bilioni 5.52.
“Agenda yako Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ya kuhakikisha wananchi wote wanajiunga na Bima ya Afya, wewe utakuwa Mkuu wa Mkoa Kinara ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia mkutano huu niwaagize wakuu wa mikoa wote wahakikishe wanakuja na mpango wa kuwasaidia wananchi wao kupitia mikakati watakayoibuni, kuwa kila mwananchi anakuwa na bima ya afya kupitia CHF iliyoboreshwa” alisema Jafo.
Awali akikagua jengo la wodi ya wazazi na jengo la upasuaji katika kituo cha Nasa Waziri Jafo amepongeza viongozi wa Wilaya ya Busega na Mkoa wa Simiyu kwa kusimamia na kuhakikisha majengo hayo yanajengwa katika viwango bora kwa kutumia “Force Account” na kuwataka wananchi kuyalinda na kuyatunza majengo hayo.
Mhe. Jafo amewataka Waganga Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanatoa huduma za afya vizuri katika maeneo yao kwa kuhakikisha kuwa wanakagua vituo vyao mara kwa mara badala ya kukaa ofisini.
Aidha, amewataka kuboresha mazingira ya vituo vyote vya afya nchini kuhakikisha vinakuwa visafi, huku akisisitiza kusimamia kufungwa kwa mfumo wa Kielektroniki wa Kukusanya Mapato, ili kuhakikisha kuwa mapato hayapotei.
Mhe. Jafo, amewataka wataalamu wa afya kuhakikisha wanakusanya na kuwa na takwimu sahihi za watoto wanaozaliwa na kufariki ili kuwezesha Serikali kuwa na takwimu sahihi zitakazowezesha kupambanana tatizo la vifo vya akina mama na watoto.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Anthony Mtaka amewashukuru wafadhili Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA), kwa namna walivyoshirikiana na Serikali katika kuchangia kuboresha huduma za afya mkoani humo, ikiwa ni pamoja na kujenga vituo vya kutolea huduma za afya.
Kuhusu mkakati wa Mkoa juu ya Bima ya Afya, Mtaka amesema “Tungehitaji kuwa ni mkoa ambao kila mwananchi atafaidika na huduma zinazotolewa na Hospitali na vituo vingine vya kutolea huduma za afya kwa kuwa na bima ya afya ili waweze kupata matibabu yao vizuri” .
Naye, Mkuu wa Idara ya Afya KOICA Tanzania Kira Thomas amesema pamoja na kufadhili ujenzi wa vituo vya afya mkoani Simiyu, mkakati wao ni kuhakikisha Zahanati 31 mkoani Simiyu zinapatiwa vifaa vya dharura kwa ajili ya kutoa huduma za dharura na kuongeza damu kwa mama wajamzito wakati wa kujifungua.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Busega Mbunge wa Jimbo la Busega Dkt. Raphael Chegeni amesema uwepo wa wodi ya wazazi na chumba cha upasuaji utatatua changamoto ya huduma za afya ya muda ya wananchi kutembea umbali mrefu kutafuta huduma na akaishukuru Serikali kwa kutenga shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya.
MWISHO
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe.Selemani Jafo akitoa maelekezo mara baada ya kukagua chumba cha upasuaji katika Kituo cha Afya cha Nasa wilayani Busega mkoani Simiyu kabla ya kukabidhiwa jengo hili lilojengwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akitoa maelezo juu ya vifaa tiba vilivyowekwa katika chumba cha upasuaji cha katika Kituo cha Afya Nasa, kabla ya jengo hilo kupokelewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe.Selemani Jafo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akitoa salamu za mkoa katika hafla ya makabidhiano Majengo ya wodi ya wazazi na chumba cha upasuaji katika Kituo cha Afya NASA pamoja na magari tisa yakiwepo matatu ya kubebea wagonjwa na magari Sita kwa ajili ya uratibu wa huduma za Afya, yaliyotolewa na UNFPA chini ya ufadhili wa KOICA mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Mkurugenzi Mkaazi wa UNFPA Bi. Jacqueline Mahon hafla ya kupokea Majengo ya wodi ya wazazi na chumba cha upasuaji katika Kituo cha Afya NASA pamoja na magari tisa yakiwepo matatu ya kubebea wagonjwa na magari Sita kwa ajili ya uratibu wa huduma za Afya yaliyotolewa na UNFPA chini ya ufadhili wa KOICA kwa mkoa wa Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka wakiteta katika hafla ya kupokea Majengo ya wodi ya wazazi na chumba cha upasuaji katika Kituo cha Afya NASA pamoja na magari tisa yakiwepo matatu ya kubebea wagonjwa na magari Sita kwa ajili ya uratibu wa huduma za Afya, yaliyotolewa na UNFPA chini ya ufadhili wa KOICA kwa mkoani humo.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Nasa wilayani Busega Mkoani Simiyu wakisikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo(hayupo pichani) katika hafla ya kupokea Majengo ya wodi ya wazazi na chumba cha upasuaji katika Kituo cha Afya NASA pamoja na magari tisa yakiwepo matatu ya kubebea wagonjwa na magari Sita kwa ajili ya uratibu wa huduma za Afya, yaliyotolewa na UNFPA chini ya ufadhili wa KOICA kwa mkoani humo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wizara ya Afya, TAMISEMI, mashirika na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu baada ya kupokea Majengo ya wodi ya wazazi na chumba cha upasuaji katika Kituo cha Afya NASA pamoja na magari tisa yakiwepo matatu ya kubebea wagonjwa na magari Sita kwa ajili ya uratibu wa huduma za Afya, yaliyotolewa na UNFPA chini ya ufadhili wa KOICA kwa mkoani humo
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa