• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Waziri Hasunga Aongeza Siku Mbili Maonesho ya Nanenane 2020

Posted on: August 4th, 2020

Kutokana  na kuchelewa kuanza kwa maonesho ya Nanenane Mwaka 2020 katika baadhi ya kanda serikali imetangaza kuongeza siku mbili za maonesho hayo ambapo kwa mwaka huu yatahitimishwa Agosti 10 badala ya Agosti 8.

Taarifa hiyo imetolewa Agosti 04, 2020 na  Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga wakati alipotembelea Banda la Chama cha wajasariamali wanawake Tanzania (TABWA) kwenye viwanja vya Maonesho ya wakulima (Nanenane) ambayo kitaifa yanafanyika Nyakabindi Mkoani Simiyu.

Hasunga amesema kuwa kulingana na mahitaji ya wadau mbalimbali na wananchi kuendelea kujifunza mbinu bora za kilimo hususani ambao hawakupata fursa awali watatumia siku hizo zilizoongezwa katika kanda zote kujionea mbinu bora za kilimo, mifugo na uvuvi na teknologia za kisasa.

“Awali tulipanga kufanya maonesho ya nanenane mwaka 2020 siku nane lakini  kutokana na maombi ya wadau na wananchi pamoja na baadhi ya kanda kuchelewa kufungua maonesho haya,  kwa mamlaka niliyopewa natangaza rasmi leo kuongeza siku mbili za maonesho, kwa hiyo tutahitimisha Agosti 10, 2020” alisema Hasunga.

Wakati huo huo mhe. Hasunga amewataka wananchi wote nchini, wakiwemo wafugaji, wavuvi na wakulima kutumia fursa hiyo ya siku zote 10 za maonesho kwenda kujifunza zaidi, teknologia mpya za kilimo, uvuvi na ufugaji.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga akizungumzia kuongezwa muda wa maonesho ya nane nane alisema amelipokea vizuri tamko hilo na watazitumia vizuri siku hizo zilizoongezwa hasa kujifunza mambo ambayo wasingeweza kuyapata pasipo kuongezewa muda huku akitoa rai kwa wakulima kujitokeza kwa wingi kufika kwenye maonesho hayo kujifunza teknolojia mbalimbali .

Kwa upande wake Luteni Kanali Peter Lushika ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya nane nane katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) akizungumza kwa niaba ya washiriki wa maonesho hayo alisema kuwa wamefurahia agizo hilo ambalo limewapa fursa ya kuendelea kutoa elimu kwa wakulima, wafugaji na wavuvi ambao hawajapata fursa hiyo.

Aidha Luteni Kanali Lushika ametoa rai kwa wananchi kutembelea banda lao kujifunza teknolojia nyingi ambazo Jeshi hilo limeandaa hatua itakayowawezesha kubadilisha mfumo wa utendaji kazi zao hatua ambayo itawasaidia kuongeza thamani kwenye mazao yao.

Aliyekuwa katibu tawala wa Mkoa wa Simiyu Jumanne Sagini amesema kuwa maonesho ya mwaka 2020 yana maboresho makubwa ya mazao na teknolojia nyingi huku akitoa rai kwa wananchi kutembelea viwanja hivyo ili kupata elimu itakayowaletea kuboresha shughuli zao za Kilimo, Mifugo na Uvuvi hatua ambayo itapelekea kuongeza tija kwenye shuguli zao.

MWISHO

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa