• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Wazabuni Watajwa Kuchangia Ucheleweshaji wa Miradi

Posted on: February 14th, 2020

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) nchini Brigedia Jenerali Charles Mbuge amesema kuwa baadhi ya wazabuni wanaouza vifaa vya ujenzi wamekuwa wakiuza vifaa kwa bei ya juu na kuchelewesha vifaa hivyo pale vinapohitajika, jambo linalopelekea baadhi ya miradi inayotekelezwa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi hilo (SUMA JKT) kutokamilika kwa wakati.

Brigedia Jenerali Mbuge ameyasema hayo Februari 13, 2020 mjini Bariadi wakati akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya ujenzi inayotekelezwa na SUMA JKT mkoani Simiyu.

Ameongeza kuwa katika kukabiliana na changamoto hiyo, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limejipanga kuanzisha maduka ya vifaa vya Ujenzi vitakavyouzwa kwa bei ya  jumla ili kuwezesha upatikanaji wa vifaa kwa urahisi, haraka na kwa bei nafuu ikilinganishwa na wazabuni wengine.

 “Tatizo moja ninaloliona kwenye utekelezaji wa miradi ni vifaa kuuzwa kwa bei ya juu sana na kucheleweshwa, tumeamua kuwa  na maduka ya vifaa ya jumla; tutatoa maelekezo kwa wakuu wa kanda za ujenzi watatupatia mahitaji yao, ili kuwawezesha kufanya kazi kwa wakati kama tunavyokubaliana na washitiri wetu,” alisema Brigedia Jenerali Mbuge.

Katika hatua nyingine Brigedia Jenerali Mbuge amesema jeshi hilo litaendelea kuwatumia vijana watakaomaliza mafunzo ya JKT katika shughuli zilizopo kwenye miradi inayotekelezwa na Jeshi hilo lengo likiwa kuwawezesha vijana hao kupata kipato na baadaye waweze kujiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa pekee.

Vile vile ameahidi kuongeza nguvu kazi ya vijana katika mradi inayotekelezwa na SUMA JKT mkoani Simiyu kuongeza kasi na miradi hiyo iweze kukamilika kwa muda uliopangwa, huku akitoa wito kwa Taasisi mbalimbali kuipa kazi SUMA JKT,  ili iendelee kuwa kutoa gawio kubwa kwa Serikali, ambapo amesema mwaka 2018/2019 ilitoa zaidi ya shilingi bilioni moja na mwaka 2019/2020 linatarajia kupanda zaidi kutokana na uwepo wa vyanzo vya kutosha.

Awali akitoa taarifa, Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya miundombinu katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mhandisi Mashaka Luhamba amesema JKT wanatekeleza miradi minne mkoani Simiyu ukiwemo wa ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, wodi ya wazazi Hospitali ya Rufaa ya mkoa, ujenzi jengo la wizara ya kilimo linalojengwa kwenye viwanja vya maonesho ya Nane nane pamoja na kiwanda cha Chaki Maswa ( Maswa chalk) .

Aidha mhandisi huyo amebainisha kuwa ujenzi wa jengo la Mkuu wa Mkoa unatekelezwa kwa kipindi cha miezi 18 kwa gharama ya shilingi bilioni 5.7 ambapo ujenzi rasmi ulianza mwezi Mei, 2019 na endapo fedha zitapatikana kwa wakati unatarajiwa kukamilika Novemba,  2020.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema ni vema SUMA JKT ikahuisha uharaka wa kutekeleza miradi kama jamii inavyoutarajia kwa kuwa jamii na Serikali imejenga imani kubwa kwa JKT kutekeleza miradi kwa wakati ikilinganishwa na wakandarasi wengine.

Mtaka ameongeza kuwa miradi inayotekelezwa na SUMA JKT iwe fursa kwa vijana waliopata mafunzo ya JKT na kumaliza mikataba yao ili waweze kupata kipato kitakachowasaidia kwenda kujitegemea na kujiajiri endapo hawataajiriwa.

MWISHO           

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/02/wazabuni-watajwa-kuchangia.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa