• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Washiriki Nanenane Kitaifa Mwaka 2020 Simiyu Wahimizwa Kuanza Maandalizi

Posted on: May 26th, 2020

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini ametoa wito kwa Taasisi, mashirika ya Umma na binafsi na wadau wote wa kilimo, mifugo na uvuvi wanaotarajia kushiriki maonesho ya Kitaifa ya Nanenane mwaka huu kuanza maandalizi ya maonesho hayo.

Sagini ameyasema hayo jana mara baada ya kukagua na kuona  hali ya maandalizi ya maonesho hayo katika Viwanja vya Nyakabindi katika maeneo ya wadau mbalimbali wa maonesho hayo.ambayo yatafanyika kwa mara ya tatu mfululizo  katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.

“Halmashauri za mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga  ambayo ndiyo inaunda Kanda ya Ziwa Mashariki zimeanza vizuri, taasisi zilizo  chini ya Wizara ya kilimo nazo zimefanya vizuri lakini baadhi ya wadau wa sekta ya kilimo hawajajitokeza; nitoe wito kwa wadau wote watakaoshiriki katika maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka huu mkoani Simiyu waweze kuja kuanza maandalizi,” alisema Sagini.

Amesema maandalizi ya vipando vya mazao, mashamba darasa, mabanda ya mifugo na mabwawa ya samaki yanahitaji muda hivyo ni vema wakaanza mapema ili kupata vitu vizuri vitakavyotumika kuelimisha wakulima, wafugaji na wavuvi kuhusu teknolojia rahisi zinazotumika katika uzalishaji wenye tija.

Mkurugenzi wa maendeleo ya mazao kutoka wizara ya kilimo, Bw. Nyasebwa Chimagu  amesema ameridhishwa na maandalizi ya maonesho ya nane nane huku akiwataka wadau kuyatumia kama kichecheo kikubwa cha ueneaji wa technolojia za kisasa katika sekta ya kilimo, mifugo na uvivu ili mazao yao yaweze kuwa na tija.

Pamoja na kukiri kuwa hamasa ya maandalizi ya maonesho ya Nanenane mwaka 2020 ilishuka baada ya kuibuka kwa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona, Chimagu amesema kuwa kwa sasa maandalizi yanaendelea katika viwanja vyote nane vya kanda za maonesho hayo nchi nzima.

Aidha Chimagu amewatoa hofu wananchi wote juu ya sintofahamu ya maonesho ya nane nane na kusema kuwa yatakuwepo na kuwasisitiza wadau ambao hawajajitokeza kujitokeza kwenye viwanja vya maonesho kwa ajili ya kuanza shughuli za maandalizi kwani tayari wengine wameanza na maendeleo ni mazuri.

"Niwatoe hofu wananchi wote nchini kuwa maonesho ya nanenane yatakuwepo kwenye viwanja vyote vya kanda,  kitaifa yatafanyika mkoani Simiyu kwa mara ya tatu mfululizo, hivyo wadau binafsi, taasisi za umma na binafsi pamoja na halmashauri ambazo bado hazijaanza maandalizi kuanza shughuli za maandalizi  ya maonesho, "alisema Chimagu.

Kwa upande wake Bwana shamba kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Ishengoma Julius amesema maandalizi ya vipando kwa ajili ya maonesho ya nane nane yamefikia 75% na vipando vya muda mfupi vimebaki kwa 25% na kusema kuwa mpaka kufikia maonesho hayo vitakuwa tayari.

Naye mkuu wa kambi ya jeshi la magereza kwenye maonesho ya nane nane Nyakabindi, Bw. Patrick Matiku amesema wanafanya ukaguzi kila siku kwenye vipando vyao ili waweza kubaini kama kuna tatizo na kulitatua mapema.

Maonesho ya Nanenane mwaka 2020 yanaongozwa na Kauli Mbiu inayosema “KWA MAENDELEO YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI CHAGUA VIONGOZI BORA 2020”.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/05/washiriki-nanenane-kitaifa-mwaka-2020.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa