NAIBU spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, ametoa medali na pesa taslimu takribani milioni 25 kwa washindi wa mashindano ya mbio za baiskeli, mbio fupi, mashindano ya ngoma za asili (Wagika na Wagalu) na uandishi wa insha kwa shule za Sekondari katika Tamasha la Simiyu Jambo Festival lililofanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu
Katika mashindano ya baiskeli wanaume (kilometa 150) Richard Laizer kutoka Arusha aliibuka kidedea na kuwa mshindi wa kwanza na kujinyakulia kitita cha shilingi 1,200,000/= , huku upande wa wanawake(KM 100 ) Laulensia Ruzuba wa Mwanza aliyekimbia km 100 na kujishindia kiasi cha shilingi 1,000,000/=.
Mshindi wa pili (wanaume)Hamisi Hussein kutoka Arusha aliyekimbia Kilometa 150 kwa saa 4:56:51 alijishindia kiasi cha Sh. Milioni 1,000,000/= ambapo mshindi wa tatu Hamisi Hatari ambaye alikimbia kwa saa 4:56:52 alipata sh.800,000.
Aidha, kwa upande wa wanawake Elizabeth Mwinamila kutoka Mkoa wa Simiyu ambaye alikimbia Km 100 kwa saa 3:10:58 alipata kiasi cha Sh. 800,000 akifuatiwa na Sophia Adson kutoka Arusha ambaye alikimbia kwa saa 3:15:47.
Kwa upande wa mbio za baiskeli walemavu washindi wote walitoka Mkoa wa Simiyu,majina yao na zawadi zikiwa kwenye mabano ni Saguda Ngulima(500,000), Emmanuel John (400,000) na Saguda Sospeter (300,000) na Mpingi Ngolo (150,000).
Katika mbio fupi kilometa 10 zilizoshirikisha wachezaji kutoka Tanzania na nchi jirani ya Kenya mshindi wa kwanza Joseph Mbatha wa Kenya alikimbia Km 10 alipata kiasi cha Sh.Milioni 1,000,000/= na medali ya dhahabu.
Nafasi ya pili ilikwenda kwa Tanzania kwa Fabian Sulle ambaye alijinyakulia Sh.800,000 wa tatu alitoka Kenya Abraham Atoo ambaye alipewa Sh. 700,000.
Kwa upande wa wanawake nafasi ya kwanza mbio fupi za Km. 10 ilikwenda pia nchini Kenya kwa Esther Chesenga ambaye alijipatia kiasi cha Milioni 1, nafasi ya pili ilikwenda Tanzania kwa Failuna Matanga ambaye alipata medali na kiasi cha sh. 800,000, nafasi ya tatu ilikwenda kwa Faith Kipsun kutoka Kenya..
Kwa upande wa wanafunzi ambao walikimbia Km 2.5 nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Saimon Marco kutoka Mkoa wa Mara ambaye alipata Sh.50,000 Lucia Mochemba kutoka Mara aliyepata pia sh. 50,000.
Nafasi ya pili ilikwenda Mkoa wa Simiyu kwa Kundi Gambo na Juma Benjamini na kupata Sh.40,000 washindi wa tatu walitoka Mkoa wa Mara kwa Veronica Samweli na Karebo Joseph, wao walipata Sh.30,000.
Kwa upande wa mbio za Km 5 washindi Mkoa wa Simiyu ulionekana kufanya vizuri zaidi ambapo nafasi ya kwanza ilishikwa na Maganda John(50,000) , Masanja Saguda(40,000) na Masaba Lameck (30,000) wasichana ni Anastazia Mkama(50,000), Asha Daniel (40,000) na Lugendo (30,000) wa Mkoa wa Mara.
Katika mashindano ya uandishi wa insha ambayo yalishirikisha shule tano za Mjini Bariadi ambazo ni Kidinda, Mahaha, Bariadi, Biashara na Simiyu mshindi wa kwanza alikuwa ni Magese Mahega(Simiyu), wa pili Liku Mayombo na wa tatu akiwa Mathias Peter.
Washiriki wa mashindano ya mbio fupi Kilometa Tano wakianza mbio hizo katika eneo la Salunda mjini Bariadi wakati wa Tamasha la SIMIYU JAMBO FESTIVAL Mjini Bariadi, ambalo limehusisha mashindano ya ngoma za asili (Wagika na Wagalu), mbio za baiskeli(Kilomita 150 wanaume na kilomita 100 wanawake), mbio fupi(Kilomita 10 na Kilometa tano), uandishi wa insha, likiwa limeshirikisha washiriki kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini, nchi jirani ya Kenya.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa