• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Wanawake, Endeleeni Kufanya Kazi kwa Bidii na Kuonyesha Mfano, Mafanikio Yenu Yasiwapelekee Kujisahau Kwamba Baba ni Kichwa Cha Familia- RC Kafulila

Posted on: March 8th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. David Kafulila ameyasema hayo wakati wa sherehe ya siku ya wanawake Duniani, ambayo kimkoa imefanyika katika wilaya ya Itilima.Mhe. Kafulila ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi ametembelea na kukagua mabanda ya wajasiriamali na kuwaagiza wakuu wa wilaya na wakungugenzi kutoa kipaumbele cha mikopo kwa wamama wajasiliamali  ambao bado hawajapata mikopo hiyo.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ,Mhe. Kafulila  amesema “ sisi sote tumetoka kwa mama, binadamu pekee ambaye hakutoka kwa mama ni Adam  pamoja na Hawa ambaye alitoka kwenye ubavu wa Adam, ambaye ni baba.Hivyo hii ni siku pekee ambayo inatupa fursa ya kutafakari safari ya mwanamke katika kutoa mchango wake kwenye taifa lake na dunia hii. Kwa uzoefu niliokuwa nao moja ya sifa kubwa ya mwananamke ni kuwa, Wanawake hawapendi kukosea, hivyo  atafanya kila kinachowezekana ili asikosee, kwa hiyo leo tunasherehekea siku ya wanawake,mama ambaye ni nguzo ya familia na viumbe wenye uvimilivu kuliko kiumbe kingine chochote duniani”.

“Wanawake ni waaminifu sana na tafiti zinaonyesha kwamba kati ya wanaume na wanawake, wanaorejesha mikopo kwa wakati ni wanawake. Hivyo Wakurugenzi na wakuu wa Wilaya katika mikopo yote mnayotoa kwa makundi ya wanawake, vijana na wenye ulemavu, mikopo kwa wanawake ipewe kipaumbele, kwani hawa wamama/dada zetu endapo wanapewa  mikopo ambayo ni mikubwa kidogo wana historia ya  kulipa kwa wakati. Mwanamke anapofanya kazi na kupata kipato anarudisha nyumbani 90%,lakini mwanaume anapeleka 35% ”. Ameeleza Kafulila.

Aidha, akizungumzia  mataifa mengine,Mhe. Kafulila ameitaja nchi ya Marekani  ambayo iliwachukua  miaka 100 kuruhusu mwanamke kupiga kura,wakati kwa nchi ya Tanzania mifumo yetu ya kisheria haijawahi kumzuia mwanamke kupiga kura. Sanjari na hayo kwa  kipindi cha mwaka mmoja wa Rais mwanamama Mhe.Samia Suluhu Hassan  amefanikiwa kuituliza nchi na kuikusanya pamoja.Anaendesha nchi kwa viwango vya juu kabisa na nchi imetulia.Mhe. Samia Suluhu Hassan amewezesha upatikanaji wa fedha za miradi kila mahali. Kwa upande wa Mkoa wa Simiyu ,Mhe. Samia Suluhu Hassan,ametoa fedha ambazo zimewezesha miradi 26 ya maji,miradi 58 ya barabara- TARURA, miradi 37- TANROADS kufanyika. Amezesha miradi 60 ya umeme kufanyika  ili kuhakikisha kuwa umeme unapatikana katika vijiji 220 kwa kipindi cha miezi 18, ili ifikapo mwanzoni mwa 2023, mkoa mzima wa Simiyu uwe na umeme.

Vilivile fedha za Mama Samia zimewezesha mkataba mkubwa wa maji wenye thamani ya Tsh. 400 bln  kufanyika mradi ambao utawezesha  vijiji 240 vya mkoa wa Simiyu kupata maji.Mhe.Rais amewezesha upatikanaji wa Tsh. 5.1bln, ambazo zinatumika katika ujenzi wa majengo 25 kwa mpigo wa  Chuo cha ufundi  VETA .Mama Samia ndio  mfano wa kuigwa  kwani amechukua mkopo mfuko wa fedha za kimataifa, mkopo wa UVIKO-19, na kuzitumia kujenga madarasa, kununua vifaa tiba, magari ya kubeba wagonjwa, mapinduzi sekta ya maji, umeme na elimu.

“Hivyo wanawake ninyi ni jeshi kubwa na mnaweza kufanya makubwa zaidi .Natamani mfanye kitu kikubwa zaidi, Kamati ya Usalama nusu ya wajumbe ni wanawake. Wabunge wengi ni wanawake, Viongozi wa Taasisi nyingi mkoa wa Simiyu ni wanawake na wanasaidia sana sababu wengi ni wachapa kazi na wanafanya kazi vizuri Sana.Mimi kama kiongozi wenu nitawapa kila aina ya ushirikiano,natamani nione jambo kubwa kuliko mikoa mingine litakaloanzishwa na kufanywa na wanawake wa Simiyu, ili  watu wengine waje kujifunza , endeleni kufanya kazi kwa bidii na kuonyesha mfano, mafanikio yenu yasiwapelekee kujisahau kwamba baba ndie kichwa cha familia”.Amesisitiza Kafulila

Aidha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Mkoani Simiyu yaliendana na utoaji wa huduma  za Upendo na faraja,ambazo zilitia ndani utoaji wa  madaftari 5000, ambayo yatasambazwa katia shule mbalimbali za mkoa wa Simiyu na pamoja na mashuka na sabuni katika kituo cha afya cha ikindilo, wilayani Itilima.

Akizungumza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Bi. Prisca Kayombo amesema ‘’wakina mama hawa kwa upendo wao wamechanga fedha ambazo zimetumika kununua madaftari 5000 ambayo yatagawiwa katika shule za wilaya zote za mkoa wa Simiyu”.Bi. Prisca Kayombo, amewaeleza washirki wa halfa hiyo kuwa, pamoja na  08/03/2022 kuwa kilele cha siku wa Wanawake Duniani kuanzia 01/03/2022 hadi 08/03/2022, shughuli mbalimbali zimekuwa zikifanywa na kina mama, hii ikiwa ni pamoja na kutoa misaada mbalimbali, kutoa elimu kwa umma, pia baadhi ya kina mama wamepewa fursa ya kupata mikopo.  “Wakina mama hawakubali kushindwa, hivyo tukiwa kama Malkia tunapaswa kung’ara na kuwa na umoja’’.Amesisitiza Bi. Kayombo.

Nae  Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Faidha Salum, amemshukuru Mkuu wa Mkoa pamoja na Katibu Tawala kwa kuiheshimisha Wilaya ya Itilima ,kwa kuipa fursa ya kuwa Wilaya Mwenyeji wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani, kimkoa. Aidha Mhe. Faidha amemshukuru sana ,Mama Samia Suluhu Hassan, kwa kuwapatia fedha ambazo zimesaidia katika miradi mbalimbali  ikiwa ni pamoja na kumtua mama ndoo kichwani. Mhe. Faidha na Wanaitilima wameahidi kushiriki kikamilifu katika suala la sensa. “Tutahakikisha tunatoa watu wote ili wahesabiwe’’. Amesema Faidha.

Aidha pamoja na wanawake wa Mkoa wa Simiyu kushiriki kwa wingi katika siku ya wanawake dunia, siku hiyo ilihudhuriwa na mwenyekiti wa  Umoja wa Wanawake (UWT-CCM)  Mkoa wa Simiyu, Mama Manyangu,Madiwani na Wabunge wanawake wa mkoa wa Simiyu.

 Akizungumza Mbunge anayewakilisha Vijana Mkoa wa Simiyu Mhe. Lucy Sabu aliwakumbusha wanawake kuwa “Mwanamke ni nuru iangazayo, mwanamke popote hakikisha kuwa unaangaza, jiheshimu, fanya kazi kwa bidii”amesisitiza Mhe. Lucy.Mwisho

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa