MKUU wa mkoa wa Simiyu,David Kafulila amewaonya wafanyabiashara wanaowakopa fedha wakulima wa zao hilo kuacha mara moja kwani wakibainika watanyang'anywa leseni ya kununua zao hilo katika mkoa huo.
Ametoa onyo hilo katika kijiji cha Mwasinasi wilayani Bariadi baada ya wananchi ambao ni wakulima wa zao hilo waliouza pamba yao kwa kampuni ya 4.C kushindwa kuwalipa na hivyo kuamua kulizuia gari la kampuni hiyo lenye namba za usajili T 534 ACZ lisiondoke kijijini hapo hadi hapo watakapolipwa.
Amesema kuwa utaratibu wa uuzaji wa pamba kwa musimu huu ni kwamba hakuna kumkopa mkulima wa pamba hivyo wafanyabiashara wanaowakopa wakulima watanyanganywa leseni baada ya kuwalipa wakulima fedha zao.
Aidha katika hatua nyingine amemwagiza Mkuu wa jeshi la polisi wilayani humo kumsaka na kisha kumkamata mmiliki wa kampuni hiyo ili aweze kuwalipa wakulima hao wamemuuzia pamna lakini hajawalipa fedha zao.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa