• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Wananchi Zaidi ya 2000 Wanufaika Na Mradi Wa Maji Simiyu

Posted on: August 15th, 2018

Zaidi ya wananchi 2000 wa Kijiji cha Lagangabilili wilayani Itilima Mkoani Simiyu wamenufaika na mradi wa maji safi na salama  na kuondokana na adha ya kutumia muda mrefu kutafuta maji kwa kusogezewa huduma ya maji karibu na makazi yao.

Hayo yamesemwa na Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, Goodluck Masige wakati akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho, aliyefika katika mradi wa maji wa Lagangabilili wenye thamani ya shilingi milioni 967, kwa ajili ya kufungua.

Masige amesema Mradi wa Maji wa Lagangabilili ulianza kutekelezwa mwaka 2015 na kukamilika mwaka 2018 na kuanza kutumika huku akibainisha  uwezo wake kuwa, una kisima chenye uwezo wa kutoa maji lita 15,000/= kwa saa, vituo vya kuchotea maji 23 na mtandao wa maji wenye urefu wa mita 29,431.

“Kukamilika kwa mradi huu wakazi  2228 wanapata huduma ya maji safi na salama kwa ajili ya kunywa na matumizi mengineyo,mradi umepunguza muda waliokuwa wanaoutumia wananchi kutafuta maji kwa kuwasogezea huduma ya maji karibu na makazi kwa saa 24,mpaka sasa kaya 25 na taasisi za Umma 20 zimeunganishiwa maji” alisema Masige .

Awali Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Benson Kilangi amesema kuwa tangu Uhuru eneo hilo lilikuwa halina maji kabisa, na baada ya kupatikana kwa huduma hiyo kutapunguza adha ya uhaba wa maji, huku akibainisha kuwa Serikali inategemea  mradi mkubwa kutoka Ziwa Victoria kuwa suluhisho la kudumu la changamoto ya maji ka ajili ya matumizi ya binadamu na wanyama pia.


Perusi Makeleja  mkazi wa Kijiji cha Lagangabilili amesema kukamilika kwa mradi huo kumewapunguzia adha wananchi hususani wanawake ya kusafiri umbali mrefu na kuamka alfajiri kufuata maji lakini umesaidia kupunguza magonjwa.

“Kabla ya mradi huu tulikuwa tunaamka usiku usiku kwenda kutafuta maji mbali tunapishana na fisi njiani, watoto wetu walikuwa wakiugua magonjwa ya tumbo na kuhara kutokana na kunywa maji ambayo hayakuwa salama, , lakini kwa sasa hizo shida hamna tena, tunamshukuru sana Rais Magufuli kwa kutuletea mradi huu sisi Wanalagangabilili” alisema

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Charles Kabeho ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kutatua changamoto za wananchi wake, ambapo katika ujenzi wa mradi huo Serikali ya Tanzania imechangia kiasi cha shilingi milioni 907 huku serikali ya Misri ikichangia kiasi cha shilingi milioni 60 ili kukamilisha ujenzi huo.

Mwenge wa Uhuru ukiwa wilayani Itilima umefungua vyumba vinne vya madarasa shule ya msingi Lagangabilili pamoja na kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa maboresho ya kituo cha afya Ikindilo unaojumuisha jengo la wodi ya wazazi, jengo la upasuaji, jengo la kuhifadhia maiti na nyumba ya mganga na kukagua Shamba darasa la Ufugaji wa Nyuki na Utunzaji wa Mazingira.

Aidha, kiongozi huyo ariridhishwa na ubora wa majengo ya miradi hiyo, huku akiwapongeza viongozi wa wilaya na Halmasharui kwa usimamizi makini ambapo aliwataka kuhakikisha majengo hayo yanakamilika ujenzi wake na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

Katika hatua nyingine akiwa Wilayani Itilima Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Kabeho  amewahimiza wananchi wa Mkoa wa Simiyu kuendelea kuchangia chakula cha mchana shuleni ili watoto wapate Muda wakujisomea zaidi hali itakayosaidia kupunguza utoro.

Mwenge wa Uhuru unaendelea na Mbio zake Mkoani Simiyu ambapo Agosti 15 Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Wilaya yaItilima umepita katika miradi sita yenye thamani ya bilioni 1.6

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI JUU YA HABARI HII FUNGUA KIPEPERUSHI HIKI:-ttps://simiyuregion.blogspot.com/2018/08/zaidi-ya-wananchi-2000-wanufaika-na.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa