• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Wananchi Wahimizwa Kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii

Posted on: September 1st, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka ametoa wito kwa wananchi Wilayani Bariadi mkoani humo kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF).

Mtaka ametoa wito huo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Ngulyati wilayani Bariadi wakati wa ziara yake yenye lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.

Amesema azma ya Serikali ni kuwa ifikapo mwaka 2020 Watanzania wote wawe wamejiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) au Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), hivyo akawahamasisha wananchi ambao bado hawajajiunga na CHF kujiunga kwa kuwa gharama yake ni nafuu.

“Watu wa Ngulyati ni wafanyabiashara wazuri, wafanyakazi wazuri, wakulima wazuri ningetamani kuwaona wote hapa mnakuwa na kadi za Mfuko wa Afya ya Jamii ambazo zinapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000, hii ni sawa na kuku mmoja tu mnapata matibabu watu sita  kwa maana ya baba, mama na watoto wa nne” amesema.

Ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuimarisha vituo vya kutolea huduma za afya ili wananchi waweze kupata huduma bora, ambapo Serikali kupitia Mradi wa RBF(Result Based Financing/Kulipa kulingana na Matokeo) imetoa fedha kwa ajili ya kuboresha huduma.

Akitoa ufafanuzi wa fedha hizo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Bariadi, Ndg.Abdallah Malela amesema, kupitia mradi wa RBF Halmashauri hiyo imepokea shilingi milioni 260, zilizogawanywa katika vituo vilivyopo 26 vya kutolea huduma za afya ambapo kila kituo kimepokea shilingi Milioni 10 ili kuboresha utoaji wa huduma za Afya.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga kufuatilia na kuhakikisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi anawasilisha kwake taarifa ya fedha za Mradi wa RBF alizopokea na kazi zilizofanyika katika vituo vya kutolea huduma.

“Mhe. DC umesikia hapa hawa watu wamepokea fedha toka mwezi saba mwaka huu na leo ndio wamekaa kikao cha mpango,  maana yake ni kwamba mwezi wa nane wananchi hawajapata huduma zilizokusudiwa na Wizara ya Afya, na naamini yanayofanyika kwenye kituo hiki yapo katika vituo vyako vyote, sasa nimuombe Mkurugenzi wa Mji Jumatatu atuletee taarifa ya  mpango uliotekelezeka” amesema Mtaka.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga amemhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kuwa atalifuatilia suala hilo pamoja na kutekeleza maelekezo yote aliyoyatoa katika ziara hiyo na ameahidi kuwachukulia hatua watumishi watakaoshindwa kutimiza wajibu wao katika kuwahudumia wananchi.

Kuhusu suala la taratibu za uwekaji wa umeme wa REA awamu ya III kwa wananchi na Taasisi za Umma ambalo liliwasilishwa na wananchi akiwemo Mwl. Daudi Jackson, Mkuu wa Mkoa, Mhe.Anthony Mtaka amesema atakutana na Meneja wa TANESCO Mkoa siku ya Jumatatu Septemba 04, ili wajadili namna na kushughulikia suala hilo.

Katika hatua nyingine Mtaka  amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi kuhakikisha Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri anafika eneo la ujenzi wa Soko la Ngulyati Jumatatu tarehe 04 Septemba kukutana na viongozi wa Kijiji na Kata, kwa ajili ya kuanza mpango wa ujenzi wa soko hilo ili kutatua kero ya ukosefu wa soko na kuwawezesha wananchi kupata sehemu ya kuuzia bidhaa zao.

Wakati huo huo Mtaka amewataka wananchi kutumia vizuri msimu wa kilimo, kulima mazao yanayostahimili ukame na akawasisitiza kutunza chakula walichokipata katika msimu uliopita kwasababu Serikali haitakuwa na chakula cha msaada.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga wakiteta jambo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa katika Kata ya Ngulyati aliyofanya kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Bariadi wakisikiliza kwa makini ufafanuzi na maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka (hayupo pichani) juu ya kero na hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wananchi wakati wa ziara yake aliyoifanya katika kata ya Ngulyati wilayani Bariadi kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Ngulyati wilayani Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) wakati wa ziara yake yenye lengo la kusikiliza kero mablimbali za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Eliasi Hopi mkazi wa Kijiji cha Nyasosi Kata ya Ngulyati wilayani Bariadi aliwasilisha kero kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) alipofanya ziara wilayani humo kwa lengo la kuzikiliza kero za wananchi na kuzitafuatia ufumbuzi.


Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa