• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Wananchi Simiyu Washukuru Serikali Kujenga Daraja Ikungulyabashashi, Wakiri Mawasiliano Usafirishaji Kuimarika

Posted on: August 17th, 2018

Wananchi wa Vijiji vya Mkuyuni, Ikungulyabashashi, Mwahalaja na Lulayu Kata ya Ikungulyabashashi, wilayani Bariadi Mkoani Simiyu wameishukuru Serikali kwa kukamilisha ujenzi wa Daraja la Ikungulyabashashi na kukiri kuwa kukamilika kwa daraja hilo kutarahisisha na kuimarisha mawasiliano na usafirishaji.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wananchi kutoka katika kata Vijiji hivyo mara baada ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho kufungua daraja hilo, wakati Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani Bariadi Agosti 17, 2018.

Wamesema awali kabla ya kukamilika  kwa daraja hilo walikuwa wakipata changamoto ya kusafirisha mazao na mifugo yao  na wakati mwingine kusafiri wao wenyewe hususani kipindi cha masika hivyo kufanya mawasiliano kuwa magumu kati ya pande mbili zinazotenganishwa na daraja hili.

“Kukamilika kwa daraja hili kutaongeza uzalishaji kwa kuwa mawasiliano ya pande zote mbili yatakuwa vizuri tofauti na mwanzo ambapo tulikuwa tunapata shida ya kusafirisha mazao yetu, mifugo  na sisi wenyewe kusafiri kutoka upande mmoja hadi mwingine hasa wakati wa masika” alisema Joshua Yakobo mkazi wa Kilalo.

 “Tunaishukuru sana Serikali kukamilisha Daraja hili ambalo litarahisisha sana mawasiliano sasa hivi wakazi wa vijiji vya Kata ya Ikunguyabashashi watakuwa wanavuka katika daraja hilo kwenda kufanya biashara katika minada ya Dutwa, Nyakabindi na Bariadi Mjini” alisema Benjamin Malala.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Kabeho alikagua ujenzi wa daraja hilo na kuridhishwa hatimaye akaupongeza Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi kwa kujenga daraja hilo kwa kuzingatia viwango.

Akisoma taarifa ya Ujenzi wa Daraja hilo Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini naVijijini(TARURA), Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhandisi. Nyamagulula Masatu amesema daraja la Ikungulyabashashi lenye urefu wa mita 16.8, upana wa mita 6.6 linajengwa kwa ufadhili wa Department For International Developments (DFID) kwa usimamizi wa TARURA.

Ameongeza kuwa ujenzi wa daraja hili utagharimu jumla ya shilingi 345,293,434/= huku akibainisha kuwa faida kuu ya mradi huu ni kurahisisha usafirishaji wa mazao ya kilimo kutoka mashambani kwa wakulima kwenda kwenye masoko.

Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi umepita katika miradi minne yenye thamani ya shilingi milioni 568 ikiwemo mradi wa maji wa Kasoli na Shule ya Msingi Otto Busese ambayo imejengwa kwa ufadhili wa Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginnery Limited kiilichopo Kasoli Bariadi.

Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Kuchambua Pamba cha Aliance Ginnery, Bw. Boaz Ogola amesema kuwa Kampuni yake inatambua kuwa nayo ni sehemu ya jamii, hivyo imeamua kushirikiana na jamii katika kuchangia maendeleo ya huduma za jamii katika elimu, afya na maji.

“Tumeshirikiana na jamii katika kuimarisha huduma za jamii,  Kasoli tumechimba kisima cha maji, tumejenga madarasa mawili na matundu matano ya vyoo katika kila shule inayotuzunguka, tumejenga Bweni la watoto wa kike katika shule ya Sekondari Mwamlapa na tunaendelea kushirikiana na jamii kuhakikisha kuwa tunaunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha elimu” amesema Ogola.

Mwenge wa Uhuru unaendelea na mbio zake mkoani Simiyu ambapo Agosti 18 utakuwa katika Wilaya ya Busega, Agosti 19 utakuwa katika Wilaya ya Maswa na Agosti 20 utakabidhiwa katika Mkoa wa Shinyanga.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/08/wananchi-simiyu-washukuru-serikali.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa