• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Wananchi Simiyu Washauriwa Kufanya Mazoezi, Kuacha Ulaji Usiofaa Kuzuia Magonjwa Yasiyoambukiza

Posted on: November 23rd, 2019

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Festo Dugange ametoa wito kwa wananchi mkoani Simiyu kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi na kuacha ulaji usiofaa kwa kuacha kutumia vyakula vyenye sukari, mafuta na chumvi nyingi na nafaka zilizokobolewa kwa lengo la kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo kisukari, shinikizo la juu la damu na saratani.

Dkt Dugange ameyasema hayo Novemba 22, 2019 wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza, ambayo ilizinduliwa rasmi kimkoa Novemba 22, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

“ Asilimia 43 ya wagonjwa wanaotibiwa katika vituo vya kutolea huduma za afya wana matatizo yanayotokana na  magonjwa yasiyo ya kuambukiza, kutofanya mazoezi kunachangia kwa asilimia 60 magonjwa yasiyoambukiza, hivyo ni vema wananchi wakafanya mazoezi na kuepuka ulaji usiofaa ili kudhibiti magonjwa haya,” alisema Dkt. Dugange.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amewataka watumishi wa idara ya afya mkoani hapa, kuwafikishia wananchi elimu ya kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza na kutoa ushauri kwa mtu mmoja mmoja kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi, lishe bora na madhara ya kutumia vilevi kupita kiasi.

Aidha, Sagini amesisitiza wataalam wa afya kuelimisha jamii namna ya kutambua magonjwa yasiyoambukiza kupitia upimaji na kufuatilia watu wenye magonjwa sugu yasiyoambukiza.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema atashirikiana na viongozi wengine kusimamia ufanyaji wa mazoezi ya viungo ikiwemo utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan la kufanya mazoezi Jumamosi ya pili ya kila mwezi ili kuwahamasisha wananchi kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza.

“Tutakachokifanya sasa hivi ni kugawa vituo vya mazoezi ya mara kwa mara kulingana na kanda kwa kuwa mji unakuwa, lakini pia tutaweka viongozi kwa kila kanda, ili kila inapofika Jumamosi ya pili mwezi viongozi wanakuja na watu wao tunajumuika pamoja katika mazoezi,”alisema Kiswaga.

Kwa upande wao watumishi walioshiriki katika mazoezi hayo wamewashukuru viongozi wa Mkoa kwa kuhamasisha watumishi na wananchi kushiriki mazoezi haya, kwa sababu wanatumia muda mwingi kazini wakiwa wamekaa hali inayoweza kuchangia wao kupata magonjwa yasiyoambukiza, hivyo wakaomba utaratibu huo uwe endelevu na waahihidi kushiriki kila wakati ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza.

“Watumishi wengi tumekuwa tukijihusisha  zaidi na shughuli zetu za kikazi tunasahau na wakati mwingine tunashindwa  kufanya mazoezi ambayo ni muhimu kwa afya zetu na ufanisi wa kazi zetu, ninashukuru viongozi wetu kuandaa na kufanikisha zoezi hili na sisi kama watumishi tunaahidi kuwa suala hili litakuwa endelevu,” alisema Marko Igenge mtumishi idara ya afya.

Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa ilizinduliwa rasmi kimkoa Novemba 22, 2019 ikiwahusisha viongozi, watumishi wa Taasisi za Umma na binafsi pamoja na  wananchi, ambapo utaratibu wa kufanya mazoezi ya viungo utaendelea kufanyika kila Jumamosi ya pili katika kila mwezi.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/11/wananchi-simiyu-washauriwa-kufanya.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa