Wito umetolewa kwa Wananchi mkoani Simiyu kujitokeza kupima Virusi vya UKIMWI (VVU) ili kujua hali za maambukizi ili wale watakaobainika kuwa na maambukizi waweze kuanzishiwa dawa mara moja na ambao watabainika kutokuwa na maambukizi kuendelea kuchukua tahadhali dhidi ya maambukizi hayo.
Wito huo umetolewa na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba wakati akitoa taarifa ya hali ya maambukizi ya VVU katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika kimkoa Desemba 01, 2020 mjini Bariadi, ambapo amebainisha kuwa pamoja na huduma za upimaji kutolewa bila malipo bado mwitikio wa upimaji ni mdogo.
“Hadi kufikia Juni 2020 ni asilimia 74 tu ya watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI katika mkoa wa Simiyu walikuwa wanafahamu hali zao za maambukizi, takwimu hizi zinaonesha kwamba katika kila wana Simiyu 100 wanaoishi na VVU, 26 miongoni mwao hawajapima kujua hali zao za maambukizi,”alisema Dkt. Kulemba.
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/12/wananchi-simiyu-wahimizwa-kupima-vvu.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa