• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Walimu Wanamazingira Simiyu Watoa Vifaa vya Kunawia Mikono Mashuleni kwa Ajili ya Tahadhari ya CORONA

Posted on: July 4th, 2020

Shirikisho la Walimu wanamazingira mkoa wa Simiyu wametoa msaada wa vifaa vya kunawia mikono ikiwa ni sehemu ya uungaji mkono juhudi za serikali mkoani hapa katika kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona.

Vifaa hvyo ambavyo vyenye thamani ya shilingi 167,000/= vimepokelewa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.  Donatus Weginah katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu mjini Bariadi Julai 03, 2020.

Akikabidhi vifaa hivyo Mwenyekiti wa shirikisho hilo, Mwalimu Aron Kiunsi amesema wameguswa kutoa msaada huo kwa viongozi wa mkoa ili wao waweze kupelekea vifaa hivyo kwenye maeneo yenye uhitaji zaidi ikiwa ni pamoja na shule ambazo kwa sasa zimefunguliwa na wanafunzi wana uhitaji wa vifaa hivyo.

Akipokea vifaa hivyo Kaimu  katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah amewashukuru walimu hao kwa kujitolea kuunga mkono nguvu ya mkoa  katika tahadhari dhidi ya Corona, huku akiendelea kutoa wito kwa wadau wengine kutoa msaada wa vifaa hivyo katika maeneo yenye uhitaji mkubwa ikiwa ni pamoja na shule.

“Ninawashukuru sana walimu kwa kutambua  mahitaji tuliyo nayo katika  kuchulua tahadhari ya Virusi vya Corona na kujitolea sehemu ya vipato vyao kununua vifaa hivi kuunga nguvu ya mkoa, sisi kama watumishi wa ofisi ya mkuu wa mkoa tutahakikisha kuwa vifaa hivi vitapelekwa katika baadhi ya shule za msingi na sekondari ambako kuna uhitaji mkubwa,” alisema Weginah.

Kwa upande wake Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju amesema anawashukuru walimu kwa kuendela kuwa wadau muhimu katika sekta ya elimu kwanza kupitia ufundishaji na pili kupitia uchangiaji huku akieleza kuwa mchango wa vifaa hivyo ambavyo vitasaidia kuwakinga na maradhi mbalimbali ikiwemo maambukizi ya Corona na kusababisha wanafunzi kusoma wakiwa salama.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk. Khamis Kulemba amesema idara ya afya mkoa iko bega kwa began a walimu hao kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanakuwa salama  ambapo ameseitiziza kuwa itasimamia kuhakikisha tahadhari zote dhidi ya ugonjwa wa COVID 19 zinazingatiwa ikiwa ni pamoja na unawaji mikono kwa maji tiririka na sabuni.

“Walimu, viongozi na jamii yote kwa ujumla twendeni tukalinde afya za watoto wetu na kulinda haki hizo ni kuhakikisha zile tahadhari zote zinafuatwa wakati wote wanapokuwa shuleni; msaada mliotoa leo ni mfano wa kuigwa kwa mtu mmoja mmoja, mashirika na taasisi mbalimbali, niwahakikishie tu kuwa tuko pamoja nanyi kuhakikisha Corona ndani ya Simiyu inatokomezwa kabisa,” alisema Dkt. Kulemba.

Naye Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM Simiyu Bw.Mayunga George amewapongeza walimu hao kwa msaada walioutoa kwa ajili ya kuwasaidia watoto kusoma kwa usalama zaidi, huku akiwapongeza pia kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuwafundisha watoto na kuufanya mkoa kuwa katika nafasi nzuri katika ufaulu ambapo amebainisha kuwa ufudishaji wao unaifanya kazi inayofanywa na serikali ya awamu ya tano katika elimu kupitia elimu bila malipo ionekane.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/07/walimu-wanamazingira-simiyu-watoa-vifaa.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa