• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Serikali Mkoani Simiyu yaja na Majibu, Upungufu wa Vitabu vya Darasa la Nne

Posted on: February 5th, 2018

Walimu wa Shule za Msingi Mkoani Simiyu wameiomba Serikali kushughulikia changamoto ya ukosefu wa vitabu vya darasa la nne ili waweze kutimiza  wajibu wao vema wa kuwafundisha wanafunzi jambo ambalo Serikali ya Mkoa imelipatia majibu.

Ombi hilo limetolewa kwa Serikali wakati wa kikao kati ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka  na walimu wa Shule ya msingi Somanda A na Somanda B ambacho kimefanyika katika Shule ya Msingi Somanda A Mjini Bariadi.

Wakiongea katika kikao hicho wamesema kutokana na kutokuwepo kwa vitabu vya mtaala ulioboreshwa wamekuwa wakitumia vitabu vya mtaala wa zamani katika kuwafundisha wanafunzi,  hivyo wanaomba serikali iwaletee vitabu vipya ili waweze kuendana na mahitaji  ya mtaala uliboreshwa.

“Wakati mwingine tunalazimika kuwafundisha watoto kwa kutumia vitabu vya mtaala wa zamani, badala ya kuwapa watoto kile wanachostahili tunawapa kilichopitwa na wakati, tunaomba tupate vitabu vya vipya ili kuendana na mtaala uliopo katika kuwapa watoto kile wanachostahili” alisisitiza Mwl.Francis Paulo kutoka Shule ya Msingi Somanda A.

Kwa upande wao wadhiti Wakuu wa Ubora wa Shule, Hellen Jackson kutoka Halmashauri ya Mji wa Bariadi na Fabian Machunde kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi wamekiri kuwepo kwa tatizo la upungufu wa vitabu vya darasa la nne jambo ambalo lina athari kwa wanafunzi hususani katika ujifunzaji .

“Ni kweli kukosekana kwa vitabu shuleni kuna athari kubwa kitaaluma mwalimu anahitaji vitabu na mwanafunzi pia anahitaji vitabu anapofundishwa darasani  na kujisomea ili kuongeza maarifa zaidi ya yale aliyojifunza darasani” alisema Hellen Jackson.

Naye Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka baada ya kuwasikiliza walimu pamoja na wadhibiti Ubora Mkuu hao, amesema Taasisi ya Elimu Ukuzaji Mitaala inapaswa kutimiza wajibu wake katika kuhakikisha inaleta vitabu hivyo katika Mkoa huo, ili walimu na wanafunzi wapate vitabu na kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

“Kama Taasisi ya Ukuzaji Mitaala Tanzania imeshindwa kuleta vitabu vya darasa la nne kwa miezi tisa sasa hawana uhalali wa kuwepo, huyo Mkurugenzi wa Taasisi anaingia Ofisini kufanya kazi gani  kama anajua nchi nzima haina vitabu vya darasa la nne, atafutwe mtu mwingine atakayekuja na maarifa mapya akubali maoni ya mikoani” alisema Mtaka.

Ameongeza kuwa ili walimu waweze kupimwa utendaji wao wa kazi ni lazima wawe na vitabu vya kufundishia na ili wanafunzi waweze kupimwa kiwango chao cha ufaulu ni lazima wawe na vitabu vya kujifunzia, hivyo ikiwa Taasisi hiyo haina uwezo wa kuchapicha vitabu hivyo kwa sasa iupelekee mkoa wa Simiyu nakala zilizohaririwa na mkoa utaweka utaratibu wa  kuchapisha vitabu hivyo.

Aidha, Mtaka amesema walimu, viongozi pamoja na wadau mbalimbali wa elimu mkoani Simiyu wamefanya jitihada kubwa katika kuboresha elimu jambo ambalo limeutoa mkoa huo kufanya vibaya katika mitihani ya Kitaifa ukiwepo wa darasa la nne, hivyo ni vema jitihada hizo zisirudhishwe nyuma kwa namna yoyote.

Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu amesema pamoja na kuwepo kwa ukosefu wa vitabu vya  darasa la nne Serikali imetoa vitabu kwa madarasa mengine ikiwemo vitabu vya najifunza kusoma  (darasa la kwanza) lakini mgawanyo wa vitabu hivyo haukuwa mzuri, akaomba ufanyike utaratibu kila mkoa upate nakala chache.

Mkoa wa Simiyu kwa sasa unahitaji vitabu zaidi ya 50,000 kwa ajili ya kufundishia na kujifunzia kwa wanafunzi wa darasa la nne.


MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI JUU YA HABARI HII FUNGUA HAPA:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/02/walimu-simiyu-waililia-serikali-ukosefu.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa