Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka ametoa wito kwa Wakuu wa Idara za Elimu Msingi na Sekondari Halmashauri za Wilaya kuisadia jamii kuondokana na mila zilizopitwa na wakati.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ametoa wito huo katika tathimini ya elimu iliyofanyika katika Shule ya Msingi Lukungu Wilayani Busega.
Ni kikao cha tathimini ya elimu Mkoa wa SIMIYU kilichowakutanisha maafisa elimu na wakuu wa idara wa Halmashauri SITA chenye lengo la kufanya taathimini ya kitaaluma na mikakati ya ufaulu wa mitihani ijayo ya kitaifa.
Akizungumza kwenye kikao hicho Mkoa wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka anasema tathimini ya matokeo ya elimu ilenge kuangalia changamoto zinazowakabili walimu sambamba na kuleta mabadiliko katika jamii.
Amesema jukumu lililombele yao ni kuhakikisha wanaibadilisha jamii ya Simiyu ili iondokane na mila potofu zilizopitwa na wakati ikiwemo ya kuwaadhibu walimu hadharani kwa kuwatandika viboko almaarufu dagashida.
Kuhusu Wilaya ya MEATU kufanya vibaya katika mitihani ya kitaifa ya darasa la saba na darasa la nne 2017 amewataka kuhakikisha wanabadilika ili kuuwezesha mkoa wa simiyu kuingia kumi bora kitaifa.
‘Meatu punguzeni kuwa mkia mnatuaibisha jitihidini muondoke huko alisema Mtaka.
Kwa upande wake Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Julius Nestory amesema pamoja na changamoto zilizopo katika sekta elimu lakini ufaulu umekuwa ukiongezeka .
Aidha amesema wametekeleza agizo la mkuu wa mkoa la kulima zao la pamba katika shule za msingi na sekondari za serikali ambapo jumla ya hekari 1,500 na hekari 230 za mahindi ili kuwawezesha wanafunzi kupata chakula cha mchana .
KUPATA PICHA ZAIDI JUU YA HABARI HII BONYEZA HAPA:https://simiyuregion.blogspot.com/2018/01/wakuu-wa-idara-elimu-wakatakiwa.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa