• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Wakurugenzi, Wakuu wa Wilaya Elimisheni Wananchi kuhusu fursa mbalimbali za Mikopo- RC KAFULILA

Posted on: January 25th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila ,ameyasema hayo leo, wakati wa hafla ya utoaji mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali vilivyopo katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi. Akizungumza,Mhe.Kafulila ameeleza lengo ya Serikali katika utoaji wa mikopo ya aina hiyo ni kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kuwapa fursa mbalimbali yakiwemo makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, kwa kuwapatia mikopo ya fedha za asilimia 10 ya mapato ya ndani yanayokusanywa na halmashauri za miji.

Fedha hizo hutokana na tozo na ushuru mbalimbali ambao hukusanywa na kuwekwa pamoja hatimaye 10% yake kutolewa kama mikopo kwa makundi maalum. "Fedha hizo ni za mikopo na sio msaada, hivyo mnawajibika kuzirejesha kwa wakati ili ziweze kukopeshwa kwa vikundi vingine, vitakavyokidhi vigezo. Nawaasa mjitahidi kuhakikisha mnatekekeleza miradi mliyoianzisha kwa ufanisi na kurejesha fedha mlizokopeshwa kama sheria, kanuni, taratibu na miongozo inavyowataka". Amesema Kafulila.

Mhe. Kafulila, amepokea hundi ya mfano kutoka benki ya NMB, yenye thamani ya Tsh. 256,090,000/-, fedha ambazo zitakopeshwa kwa jumla ya vikundi 53 vyenye wanufaika 364 kwa awamu ya kwanza katika mwaka wa fedha 2021/2022. Fedha hizo zitagawanya kwa makundi maalum vikiwa na mchanganuo ufuatao, wanawake vikunndi 37 watakopeshwa kiasi cha Tsh.180,100,000/-, vijana vikundi 11 vitakopeshwa Tsh.49,420,000/- na watu wenye ulemavu vikundi 5 watakopeshwa Tsh. 26,570,000/-.

Akizungumzia changamoto wanazokabiliana nazo katika utoaji wa mikopo ya 10% , Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bariadi Mji. Bw. Adrian Jungu, amezitaja changamoto hizo kuwa, mapato ya ndani kuwa madogo ikilinganishwa na mahitaji ya makundi maalum ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu ambao wanaotakiwa kukopeshwa, baadhi ya vikundi kukosa uaminifu katika kurejesha mikopo, baadhi ya vikundi kubadilisha matumizi ya fedha walizokopeshwa kulingana na miradi waliyoombea mikopo, badala yake kugawana fedha au kuanzisha miradi mipya ambayo hawana uzoefu nayo na hivyo kushindwa kurejesha mikopo hiyo.

Aidha Mkurugenzi huyu ameeleeza mikakati mbalimbali ambayo Halmashauri ya Bariadi Mji imejipanga kufanya ili kukabiliana na changamoto hizo ikiwa ni pamoja na kuendelea kubuni vyanzo vipya vya mapatoo ili kuongeza mapato ya ndani, kuboresha mbinu za ukusanyaji mapato kwenye vyanzo vilivyopo,kuendelea kutoa elimu kwa vikundi ili viiweze kuzingatia taratibu na miongozo iliyowekwa na kufuatilia marejesho ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani wadaiwa sugu. Hadi sasa, mashauri 6 ya madai yamefunguliwa mahakamani na tayari vikundi 2 kati ya 6 vilivyoshtakiwa  vimelipa na kumaliza deni walikokuwa wanadaiwa. Halmashuri ya Bariadi Mji inadai kiasi cha Tsh. 35,057,450/- kutoka kwenye vikundi 15.

Ili kuhakikisha ufanisi katika utoaji wa mikopo hiyo Mhe Kafulila amewaagiza wakurugenzi wote wa halmashauri na wakuu wote wa wilaya za Mkoa wa Simiyu kuwahamasisha na kuwaelimisha wananchi ili waelewe na waitumie fursa hiyo kwani kuna watu wengi ambao hawajui kuhusu fursa hizo. Aidha amewataka wakuu hao kutumia zoezi la upandaji miti kuwa kigezo kimojawapo cha kupata mkopo. Wanakikundi wanatakiwa wapande miti ama ya kivuli ama ya Matunda na kuonyesha eneo walilopanda miti hiyo kisha ndio wapewe mkopo, hii itaharakisha na kurahisiha sana Simiyu ya Kijani.

Aidha Mhe Kafulila amewataka viongozi hao kujua watu wao wanajishughulisha na nini. "Jengeni dhana pana ya uelewa juu ya shughuli mbalimbali wanazofanya wananchi wa eneo lenu.Maafisa biashara wote ni jukumu lenu kuvijua vikundi vyote vinavyohusika na Mikopo.Maafisa biashara wote ni lazima muwe walezi wa vikundi hivi".Amesisitiza Kafulila.

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa