• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Wahamiaji Haramu Wakamatwa Mkoani Simiyu

Posted on: December 2nd, 2020

Idara ya Uhamiaji kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limewakamata wahamiaji haramu raia wa Ethiopia wapatao 34 katika kitongoji cha Mwalukonge Kijiji cha Lamadi wilayani Busega.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo Desemba 02, 2020 katika Kituo cha Polisi cha Lamadi, Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Simiyu, Mariam Mwanzalima amesema wahamiaji haramu hao wamekamatwa  Desemba 02, 2020 na askari  waliokuwa doria .

“ Katika maelezo yao wanasema wametokea Kenya walikuwa wanaelekea  Malawi wakisindikizwa na Wakenya wawili, walipofika Lamadi ilitokea purukushani kati yao na wasindikizaji wao baada ya kuwalazimisha kupanda kwenye mitumbwi ili watembee nao ziwani; ndiyo wakakimbia na kuelekea mashambani, bahati nzuri askari wetu walikuwa doria wakafanikiwa kuwakamata” alisema Mwanzalima.

Ameongeza kuwa wahamiaji haramu hao watafikishwa mahakamani kwa kuwepo nchini kinyume cha sheria ya Uhamiaji Sura ya 54 rejeo la mwaka 2016 kifungu cha 4 hukumu yao ikiwa ni kifungo kisichopungua miaka miwili, huku akibainisha kuwa Vyombo vya usalama vinaendelea kuwatafuta wasindikizaji wa wahamiaji hao na watakapokamatwa watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Aidha, Mwanzalima ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu kufanya kazi zitakazowaingizia kipato halali na kuwaonya wasijiingize katika biashara haramu ikiwemo ya kusafirisha wahamiaji haramu jambo ambalo linaweza kupelekea wao kushtakiwa,  nyumba na vyombo vya usafiri vitakavyotumika katika biashara hiyo kutaifishwa.

“Natoa onyo kwa Mtanzania yeyote aliyeko Mkoa wa Simiyu atakayejishughulisha kuwasaidia, kuwaonyesha njia ya kwenda popote tukimkamata sheria inasema atafungwa kifungo kisichopungua miaka 20, atakayewahifadhi kwenye nyumba yake atafungwa na nyumba itataifishwa na serikali; ambaye chombo chake kitatumika kuwasafirisha atafungwa miaka 20, atalipa faini isiyopungua milioni 20 na chombo chake kitataifishwa,” alisema Mwanzalima.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga amewataka wananchi kuwa makini na kuhakikisha kuwa wageni wanaoingia katika maeneo yao wanawafahamu na ikitokea kuna watu wanaowatilia shaka  watoe taarifa kwa viongozi walio katika mamlaka zao za utawala na viongozi hao washirikiane na  vyombo vya usalama ili hatua zichukuliwe haraka.

Mmbaga ametoa wito kwa vijana wa Mkoa wa Simiyu kutumia fursa ya amani iliyopo hapa nchini kuendelea kutumia fursa za kiuchumi zilizopo kufanya kazi zitakazo waingizia kipato halali na katu wasijiingize kwenye biashara haramu, huku akibainisa kuwa mkoa huo hautawafumbia macho wote watakaojihusisha na vitendo vya biashara haramu.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, ACP. Richard Abwao ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi pale watakapowaona watu wasiowatambua katika maeneo yao ili kuendelea kuimarisha ulinzi wao pamoja na mali zao katika maeneo waliyopo.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/12/wahamiaji-haramu-wakamatwa-mkoani-simiyu.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa