• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Waganga Wafawidhi Watakaoshindwa kusimamia Vituo Vyao Kuvuliwa Madaraka

Posted on: June 4th, 2018

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Jumanne Sagini amewaagiza Waganga Wakuu wa Wilaya kuwaondoa katika nafasi za usimamizi wa zahanati na vituo vya afya ,waganga wafawidhi watakaoshindwa kusimamia vituo vyao kufika vigezo vilivyowekwa katika utoaji huduma za afya kwa wananchi kupitia mpango wa malipo kwa ufanisi (RBF).

Agizo hilo amelitoa wakati wa kikao chake na Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa wilaya, Timu ya Usimamizi wa Huduma za Afya Mkoa(RHMT), waganga wafawidhi wa zahanati na vituo vya afya lengo likiwa ni kujadili matokeo ya Mpango wa Malipo kwa ufanisi (RBF) kwa kipindi cha Mwezi Januari-Machi 2018 na masuala mbalimbali yahusuyo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ikiwepo Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa.

“Waganga na Wauguzi wafawidhi tumewaita hapa tunataka mabadiliko kwenye utendaji wenu, vituo vyenu wote viende kwenye Alama A, kinyume na hapo Waganga Wakuu wa Wilaya wawavue madaraka na Waganga wakuu wa Wilaya wasipofanya  hivyo Wakurugenzi washughulikieni wao” alisema Sagini.

Amesema kutotekeleza majukumu yao vizuri ikiwa ni pamoja na kushindwa kusimamia suala la ujazwaji wa  takwimu sahihi kwa wakati,  kunasababisha Vituo vyao kutopata fedha za mpango huo (RBF)  ambazo hutolewa kwa vituo vinavyofanya vizuri,  ambapo vituo hivyo vikizipata zitasaidia kuboresha miundombinu ya Afya na ununuzi wa dawa na vifaa tiba.

Ameongeza kuwa  Timu za Usimamizi wa Huduma za Afya Wilaya (CHMT) zinapaswa kufanya ufuatiliaji na usimamizi katika Vituo vya kutolea huduma na kuhakikisha mapungufu yote yanayojitokeza yanafanyiwa kazi ili vituo vyote vitoe huduma kwa ufanisi na kupata fedha kulingana mwongozo wa Mpango wa RBF ambazo zitasaidia kuboresha huduma kwenye vituo.

Katika hatua nyingine Sagini amewataka Waganga wakuu wa Wilaya na Waganga Wafawidhi wa Vituo vya kutolea huduma za Afya kuwasilisha taarifa za wagonjwa wanaopata huduma kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya  kwa wakati kama maelekezo yanavyowataka kufanya ili kuondoa usumbufu usio wa lazima.

Nao Wasimamizi wa Vituo baada ya maelekezo ya Katibu Tawala wa Mkoa wamekiri kuwa watabadilika na kuhakikisha vituo vyao vinafanya vizuri na kufikia alama A ili kuwawezesha kupata fedha kupitia Mpango wa Malipo kwa Ufanisi(RBF) zitakazowasaidia kuboresha huduma za afya katika vituo vyao.

“ Nimesikitishwa sana na Halmashauri yetu kukosa fedha za RBF kiasi kilichotajwa na mratibu kwa sababu ya baadhi ya watendaji kutotimiza wajibu wao, mimi ninaona haya yote yako ndani ya uwezo wetu, kuanzia sasa tunapaswa kutimiza wajibu wetu na tuhakikishe taarifa zote zinazopelekwa wilayani zinajazwa kwa usahihi na kwa wakati” alisema Godfrey Pascal kutoka Zahanati ya Nkololo

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw.Fabian Manoza amesema ipo haja ya kuwajengea uwezo na kutoa mafunzo ya menejimenti ya takwimu  kwa wasimamizi wa vituo vya kutolea huduma za Afya, ili waweze  kukusanya takwimu zinazotakiwa kwa mujibu wa mwongozo wa Mpango wa RBF hatimaye vituo vyao vipate alama nzuri na fedha zitazowasaidia kuboresha huduma.

Kwa upande wake Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Simiyu Jarlath Mushashu ameziomba Halmashauri zote Mkoani Simiyu kulipa deni ambalo Mfuko huo unazidai lililofikia shilingi milioni 78, ili kuuwezesha mfuko huo kutoa huduma za matibabu kwa wanachama na wategemezi wao kama inavyotakiwa.

Wakati huo huo Mushashu amewaomba Wakurugenzi wa Halmashauri kuwasilisha kwa wakati michango ya watumishi ya Bima ya Afya hususani watumishi wanaolipwa kwa kutumia mapato ya ndani ya Halmashauri.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/06/waganga-wafawidhi-watakaoshindwa.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa