• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Wafanyabiashara Wahimizwa kusajili Biashara BRELA Zitambuliwe, Zifanywe Kwa Ushindani

Posted on: April 19th, 2019

Wafanyabiashara hapa nchini wametakiwa kusajili biashara zao kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ili ziweze kutambuliwa kirahisi na  waweze kufanya biashara kwa ushindani wa Kitaifa na Kimataifa.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wafanyabiashara Mjini Bariadi Mkoani Simiyu mara baada ya kutembelewa na Maafisa kutoka BRELA katika maeneo yao ya biashara kwa lengo la kufuatilia masuala mbalimbali ya Wakala huo ikiwa ni pamoja kutoa elimu na kuangalia mwitikio wa mfumo wa usajili wa biashara kupitia mtandao (Online Registration System-ORS).

“ Kuna faida sana kwa mfanyabiashara kusajili biashara yake BRELA kwanza inatambulika, usajili pia utamsaidia kupata urahisi hasa kwa makampuni yanayotaka kuingia mkataba na yeye, akihitaji huduma za kifedha katika benki na utamsaidia kutangaza biashara yake popote”

“Kampuni yoyote inayotaka kuingia mkataba na sisi ni lazima inaomba nyaraka za usajili wa BRELLA, tukitaka huduma za kifedha kwenye benki nao wanahitaji nyaraka za BRELA, yapo manufaa makubwa kusajili BRELA” Lucy Sabu Mkurugenzi Msaidizi, Hoteli ya Sweet Dream Bariadi.

Naye Bi Neema Joseph Meneja wa Kituo cha mafuta JBS Bariadi ameshukuru BRELA kwa kuanzisha usajili wa biashara kupitia mtandao(Online Registration System-ORS) jambo ambalo amesema litawawasaidia wafanyabiasha kufanya usajili mahali walipo badala ya kusafiri kufuata huduma hiyo Dar es salaam kama ilivyokuwa awali.

Aidha, Bi. Neema ameomba BRELA iendelee kutoa elimu kuhusu umuhimu wa usajili wa biashara kwa wafanyabiashara na matumizi ya mfumo mpya wa usajili kupitia mtandao ili uweze kufahamika vizuri zaidi kwa wafanyabiashara.

Mkurugenzi wa Utawala na Fedha kutoka BRELA, Bw. Bakari Mketu amesema mara baada ya kutoa elimu ya usajili miezi miwili iliyopita kiwango cha usajili kimeongezeka na kufikia asilimia 80 ya lengo walilojiwekea kwa robo zote tatu ndani ya mwaka .

“Tumesajili kampuni 4678 zaidi ya 66% huku malengo yakiwa kusajili 7110 na kusajili majina ya biashara 8022 zaidi ya 49% huku malengo yakiwa kusajili majina 1640 kwa robo zote tatu .... kwanza tulikuwa tunapanda taratibu ...tutaendelea kuwaelimisha wateja wetu ili kuhakikisha wateja wote wanakuwa uelewa wa kutosha.

Katika hatua nyingine Mketu ametoa rai kwa wanasheria kuzingatia sheria katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwa ni pamoja na masuala yanayohusiana na Usajili, ili kuepuka usumbufu kwa wafanyabiashara.

‘’Sheria ni taaluma ambayo bado inaheshimika sana, kujifunza kila siku ndio taaluma inavyotaka sisi hatuwezi kuwafundisha kazi…lakini tunaomba wazingatie sheria wakati wakifanya majukumu yao, mathalani kuna mwanasheria alifanya zoezi la kubadili hisa za mteja (share transfer) pasipo kufuata utaratibu ambao umeainishwa kisheria na TRA”  alisema Mketu.

Naye Suzana Senso kutoka BRELA amesema ni vema Wanasheria wanapofanya kazi kujiridhisha kwanza juu ya taratibu na sheria zinazotakiwa kufuatwa katika kazi husika ili waweze kuwasadia wateja wao kwa kuzingatia sheria na taratibu.

“Naomba nitoe rai kwa wanasheria, ukipata kazi uliza  wengine taratibu zilivyo  ili uweze kumsaidia mteja, huyu mama alitaka kuhamisha hisa (share transfer) mwanasheria akaja akachomoa nyaraka na kuweka nyingine akamweleza kuwa utaratibu umekamilika wakati utaratibu ulipaswa ufanyike TRA; kutokana na uelewa  wa mama na afisa biashara mkoa wao walitutafuta, najiuliza ni wangapi wanakutana na changamoto hizi” alihoji Bi. Suzan Senso.

Aidha, Bi. Elizabeth Samweli kutoka Kampuni ya Mlashi General Supplies alikiri kukumbwa na changamoto hiyo ya  mwanasheria kufanya zoezi la kuhamisha hisa pasipo kufuata utaratibu uliowekwa kisheria na kushukuru BRELLA kwa namna walivyomsaidia mara baada ya kuwaeleza changamoto hiyo; huku akisisitiza BRELA kuendelea kutoa elimu.

Maafisa kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wako Mjini Bariadi Simiyu kwa ajili ya kuendelea kutoa elimu juu ya usajili wa biashara kwa wafanyabiashara mkoani hapa pamoja na wajasiriamali walio katika Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Waadventista Wasabato(ATAPE) ambao unafanyika Mkoani Simiyu.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/04/wafanyabiashara-wahimizwa-kusajili.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa