• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Viongozi, Wananchi na Wadau Simiyu Watakiwa Kushirikiana Kukamilisha Ujenzi wa Madarasa

Posted on: December 13th, 2020

Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.  Anthony Mtaka amewataka viongozi wa kisiasa kushirikiana pamoja na viongozi serikali na wadau wengine wa elimu katika kuhakikisha ujenzi wa madarasa unakamilika mapema, lengo likiwa kuhakikisha wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza wanapata madarasa ya kusomea.

Mtaka ameyasema hayo  Desemba 12,2020 kwenye kikao kazi cha mkoa cha kujadili uelekeo wa mkoa wa Simiyu katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2020/2025 ) katika masuala mbalimbali ikiwemo afya,elimu,kilimo,viwanda na ajira kwa vijana, ambacho kimewashirikisha viongozi wa chama na serikali, ,wafanyabiashara ,viongozi wa dini ,taasisi za umma na binafsi na wadau wa maendeleo wa Mkoa, kilichofanyika Mjini Bariadi mkoani Simiyu.

“Simiyu kipaumbele chetu cha kwanza ni elimu, nimekuwa nikiwaambia watu wa Simiyu tukitaka kushindana tusomeshe watoto, malizieni maboma ya madarasa watoto wapate mahali pa kusomea, kila mmoja abebe kwa uchungu jambo hili kuona madarasa yanakamilika lakini mkienda  kwenye mabaraza mkaanza kubishana hamtawasaidia wananchi,” alisema Mtaka

Aidha Mtaka ameongeza kuwa kwa maeneo ambayo yana madini pamoja na maeneo yanayonufaika na uhifadhii kama vile vijiji vya Makao, Mwangudo na vingine Wilayani Meatu, wananchi wasichangishwe badala yake asilimia zinazotolewa kwa ajili ya vijiji zielekezwe kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Ameongeza kuwa mkoa huwa umejiwekea malengo ya kuongoza katika mitihani yote ya Taifa ambapo amewataka viongozi wa Serikali kuendelea kutoa motisha kwa walimu ikiwa ni pamoja na kuacha kutoa lugha za kuwaudhi na kuwakera walimu ili waendelee kufanya kazi kwa moyo.

Sambamba na hili Mtaka ametoa rai kwa Madiwani wote wa Mkoa huo kuacha tabia ya kuazimia watumishi wao kwa kuwa hali hiyo inawavunja moyo watumishi badala yake waweke mazingira ya watumishi kupenda kazi na ikiwa watumishi watafanya jambo lisilotakiwa wawasiliane na mamlaka nyingine ili waweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu.

Katika hatua nyingine Mtaka amesema Simiyu Imejipanga kuanzisha utaratibu mpya wa utoaji wa mikopo nafuu itokanayo na asilimia 10 ya mapato ya ndani inayotolewa kwa vijana wanawake na walemavu, akibainisha kuwa fedha hizo zitatangazwa na kushindaniwa; ambapo vikundi havitapewa fedha badala yake Halmashauri zitalipia teknolojia zinazohitajika kupitia SIDO na sehemu ya fedha inayobaki itatumika kuwajengea uwezo wahusika wa vikundi hivyo.

Awali akitoa taarifa ya elimu mkoani hapo kwa niaba ya afisa elimu mkoa wa Simiyu , Jusline Bandiko amesema mkoa huo una mahitaji ya vyumba vya madarasa 565 ,vilivyopo ni 419 huku upungufu ukiwa vyumba 155 ambavyo vinatakiwa kukamilika kwa ajili ya kidato cha kwanza 2021.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simyu, Mhe. Enock Yakobo ametoa wito kwa viongozi kuona umuhimu wa kuanzisha mfuko wa elimu wa mkoa na kuwahamasisha wananchi kuchangia mfuko huo ili uweze kusaidia katika ujenzi wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu na ununuzi wa viti na madawati.

Miriam Mmbaga ni Katibu Tawala wa Mkoa huo ametoa wito kwa viongozi wa Umma mkoani Simiyu kufanya kazi kwa kuzingatia miongozo, sheria na taratibu na kwa uadilifu mkubwa wakijiepusha na masuala ya migongano ya maslahi katika maeneo yao, huku akisisitiza wafanye maamuzi sahihi kwa wakati sahihi kwa maslahi ya wananchi wanaowaongoza.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Kheri James ambaye pia ni Mlezi wa CCM kwa mikoa ya Simiyu na Mara amesema jamii inahitaji mageuzi ili kufikia mageuzi hayo inapaswa kuwa na viongozi wenye uthubutu na ujasiri, huku akitoa wito kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu kufanya kazi kwa ushirikiano na kutumia vizuri madaraka, mamlaka na ushawishi walio nao kwa manufaa ya wananchi wanaowaongoza.

MWISHO

 KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/12/viongozi-wananchi-na-wadau-simiyu.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa