• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Viongozi, Wabunge wa Mkoa wa Simiyu wakutana Dodoma kujadili Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda

Posted on: May 6th, 2017

 Viongozi wa Mkoa wa Simiyu,  wamekutana na Wabunge wa Mkoa huo mjini Dodoma katikakikao maalum  kujadili na kupata uelewa wa pamoja juu ya Ujenzi wa Uchumiwa Viwanda Mkoani Simiyu.

Pamoja na kujenga uelewa wa pamoja kwa wadau hao kuhusu Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Mkoani Simiyu, kikao hicho piakilikusudia kupata baraka za Wabunge wa Mkoa huo juu ya miradi ya uanzishwajiwa Viwanda katika Halmashauri zote sita.

Katika kikao hiki  wajumbe wamepata fursa ya kupitia maandiko ya miradi ya uanzishwaji wa viwanda yaliyowasilishwa na Wakurugenzi wa Halmashauri zote sita; viwanda ambavyo vitajengwa katika maeneo tofauti ya Mkoa wa Simiyu chini ya utekelezaji wa  Kauli Mbiu ya "Wilaya Moja Bidhaa Moja".

Miradi iliyowasilishwa ni pamoja na upanuzi waKiwanda cha kutengeneza Chaki wilayani Maswa, Upanuzi wa kiwanda cha kusindikamaziwa wilayani Meatu ambapo kiwanda hicho kitaongeza uzalishaji wamaziwa   yakiwemo maziwa ya unga.

Miradi mingine ni ujenzi wa kiwanda chakutengeneza vifungashio wilayani Maswa,kiwanda cha kutengeneza sabuni zamaji,miche na za unga wilayani Itilima, kiwanda cha kutengeneza Tomato sauce naChill sauce Busega, kiwanda cha kusaga nafaka na kupaki unga katika Halmashauriya Mji wa Bariadi na kiwanda cha kuchakata ngozi na bidhaa za ngozi katikaHalmashauri ya Wilaya ya Bariadi.

Wabunge wa Mkoa wa Simiyu chini ya Uenyekitiwa Mbunge wa Bariadi,Mhe.Andrew Chenge kwa pamoja wamepongeza juhudizinazofanywa na viongozi na watendaji mkoani humo na kuunga mkono miradi yoteya uanzishwaji wa Viwanda , ambapo hatua inayofuata sasa ni kufanyika kwaUpembuzi Yakinifu kwa miradi hiyo na kuanza utekelezaji.

Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa waSimiyu Mhe Anthony Mtaka amesema Serikali mkoani humo imedhamiria kuhakikishaazma ya Serikali ya awamu ya tano ya Sera ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda inatekelezwa kwa vitendo.

Naye Katibu Tawala Mkoa,Ndg Jumanne Saginiamesema Wataalam kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii ya (ESRF)wataanza kufanya upembuzi yakinifu wa mradi wa upanuzi wa kiwanda chakutengeneza chaki na watakamilisha katika kipindi cha wiki wiki mbili, wakatiupembuzi yakinifu kwa miradi mingine utafanywa na kukamilika katika kipindicha  miezi miwili.

Kikao hiki kimehusisha baadhi ya wajumbe yaKamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa,Wabunge wa Mkoa huo, Wakurugenzi wa Halmashauri,Wenyeviti na Makamu wenyeviti wa Halmashauri, Maafisa Mipango na Wanasheria waHalmashauri zote za mkoa huo,wataalam wa masuala ya Viwanda pamoja na wadauwengine wa Uwekezaji kutoka NSSF.

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa