Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Ndg. Jumanne Sagini amewataka viongozi wa dini kwenda kuwa chachu ya kuibadilisha jamii , kuhusu matumizi ya nishati na maji ,na namna ya kutoa taarifa wanapouziwa bidhaa isiyo na kiwango .
Sagini ametoa ushauri huo alipokutana na viongozi hao mjini bariadi ,ikiwa ni mwendelezo wa Baraza la Ushauri watumiaji Nishati na Maji kuyafikia makundi mbalimbali kueleza umuhimu wa chombo hicho. .
Sagini amesema viongoni wa dini ni watu muhimu katika jamii ,hivyo ni vema elimu waliyoipata wakaitumie katika kupunguza changamoto za nishati na maji kwa kutumia ujumbe mbalimbali
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la watumiaji Nishati na Maji Getruda Mbilinyi amesema kuwa kukutana na kundi la viongozi wa dini ambao wanaushawishi mkubwa katika jamii itasaidia wananchi wengi kuzijua haki zao ,pale wanapopata huduma zisizoridhisha
Baadhi ya viongozi wa dini wamesema kuwa mafunzo hayo waliyoyapata watayatumia kuwaelimisha waumini wao kupitia mahubiri faida za utumiaji nishati hiyo.
Mafunzo kwa viongozi wa dini yaliyokuwa ya siku moja yaliyoandaliwa na Baraza la Ushauri , Watumiaji wa huduma za Nishati na Maji baina ya viongozi themanini na mbili wa dini na Kamati ya watumiaji wa huduma ya nishati na maji ,halmashauri ya mji wa bariadi ,lengo likiwa utoaji elimu kuhusiana na upatikanaji wa huduma bora kwa wateja.
KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII FUNGUA HAPA:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/04/viongozi-wa-dini-watakiwakuwa-chachu-ya.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa